Taasisi za Sekta Binafsi zimekumbushwa kuwasilisha kwa wakati na usahihi michango ya waajiriwa wao katika Mfuko wa hifadhi ya jamii Zanzibar ZSSF ili kutimiza lengo la kuwawezesha kuwa na hifadhi endelevu ya maisha yao.
Akizungumza katika Mkutano wa Nane Wadau wa ZSSF, katibu Mkuu Wizara ya Nchi Afisi ya Rais kazi uchumi na uwekezaji anaeshughulikia uchumi na uwekezaji, Khamis Suleiman Mwalimu amesema kuna baadhi Waajiri wa Sekta Binafsi wanafanya udanganyifu katika kuwasiilisha Michango ikiwemo kutowasajili wafanyakazi wote katika Mfuko wa ZSSF au kuwasilisha kiwango tofauti na Mishahara halisi ya Wafanyakazi hali inayowanyika haki yao wanapostaafu ama wanapopatwa na Majanga.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa ZSSF Nassor Shabaan Ameir amesema Mfuko huo tangu kuanzishwa kwake Miaka 25 iliyopita umepiga hatua ikiwemo kuongezeka thamani ya Mfuko kwa Asilimia 60.
Kauli Mbiu ya Mkutano huo ni taarifa sahihi za Mwajiri na Mwajiriwa ni chachu ya Mafao bora.