SERIKALI IMESEMA HAIJAWEKA REHANI CHOCHOTE KUPATA MKOPO WA BILIONI 2.5 KUTOKA SERIKALI YA KOREA

RIPOTI YA MIKOPO

    Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema haijatoa wala kuweka rehani kitu chochote kwa ajili ya kupata Mkopo wa Dola za Marekani Bilioni 2 Nukta 5 kutoka Serikali ya Jamhuri ya Korea.

    Akitoa Ufafanuzi kuhusu Mkopo wa Dola za Marekani Bilioni 2.5, sawa na Shilingi Trilioni 6.7 ambao Tanzania umeupata kutoka katika Serikali ya Jamhuri ya Korea Msemaji Mkuu wa Serikali Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Mobhare Matinyi amesema Mkopo huo ni wa Masharti Nafuu na unalenga kufadhili Miradi muhimu ya maendeleo kwa Kipindi cha Miaka Mitano Ijayo kuanzia Mwaka (2024 Hadi 2028).

    Amebainisha kuwa Mkopo huu ni Sehemu ya Makubaliano katika Awamu ya Pili ya ushirikiano wa Miaka Mitano Ijayo na utakaolipwa Katika Miaka 40 kwa Riba ya 0.01%.

    Mkurugenzi Matinyi amezitaja faida za Mkopo huo kuwa ni kusaidia kufadhili Miradi muhimu ya Maendeleo ikiwemo ya miundombinu, Elimu, Afya, na Nishati, Miradi ambayo itaboresha huduma za Kijamii na kuinua kiwango cha Maisha cha Wananchi.

    Ufafanuzi wa Taarifa ya Mkopo kutoka Serikali ya Jamhuri ya Korea ulitolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali umekuja kufuatia upotoshaji uliotokea katika Taarifa za baadhi ya Vyombo vya Habari zilizosambaa hapo Jana kuhusu Mkopo huo ambao umesababisha taharuki kwa Watanzania.   

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Samia Suluhu Hassan yupo Ziarani Nchini Jamhuri ya Korea, Ziara ambayo itatamatika Juni 6, 2024                                   

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.