SMZ KUENDELEA KUIMARISHA VIWANJA VYA NDEGE

DR KHALID SALUM MOHAMMED

Serikali inafikiria kujenga Jengo la Nne la Abiria ili kurahisisha huduma za usafiri wa Anga Nchini.

Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Dkt. Khalid Salum Muhamed katika mazungumzo yake na ujumbe wa Watu 9 kutoka Benki ya Exim ya China ukiongozwa Mkurugenzi Mkuu wa masuala ya usafiri wa Benki ya Exim ya China Chen Zhen, amesema lengo ni kuona wanashirkiana katika masuala ya Miundombinu.

Amesema ujio wa Ujumbe huo pia utatoa fursa ya Ushirikiano katika Miradi ya ujenzi ikiwemo Bandari. 

Katika hatua Nyenginedkt. Khalid amesema Zanzibar inafunguka Kiuchumi kupitia Bandari, Viwanja vya Ndege na Barabara na itawezesha kukuza ustawi na fursa za ajira kwa Jamii.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.