SERIKALI KUENDELEA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI KWA WATU WENYE ULEMAVU

MAKAMO WA PILI

     Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Jumuiya ya Wasioona Zanzibar (ZANAB) na Jumuiya nyengine za Watu wenye Ulemavu ili kuhakikisha inaweka mazingira wezeshi yatakayowasaidia Watu wenye Ulemavu kufaidika na fursa mbali mbali Nchini.

    Kauli hiyo ni ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, katika Hotuba yake iliyosomwa na Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Hemed Suleiman Abdulla wakati wa kuahirisha Maadhimisho ya kuongeza uwelewa kwa Jamii juu ya Watu wenye Ulemavu yaliyofanyika Mto wa Pwani Wilaya ya Kaskazini 'a' amesema Serikali inawathamini na imetenga Shilingi Bilioni 1 Nukta 2 zimetenga kwa Mwaka wa Fedha 2024-2025 kwa ajili ya kuendeshea Mabaraza ya Wilaya ya Watu Wenye Ulemavu.

    Aidha amesema Serikali itahakikisha sheria ya Watu wenye Ulemavu inafanyiwa kazi na kupelekwa Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kujadiliwa na hatimae kupitishwa kuwa sheria kamili ambayo itatoa miongozo mbali mbali kwa Taasisi na Jumuiya za Watu wenye Ulemavu kufanikisha malengo waliyojipangia.

     Akizungumza kwa Niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na uchukuzi Mhe. Dkt.Khalid Salum Muhammed amesema Serikali zote mbili zimefanya mapitio ya Sera na sheria kuhakikisha Watu wote wanapata haki sawa ikiwa ni pamoja na Makundi maalum katika nyanja zote za Kiuchumi na Kijamii.

    Akisoma Risala iliyoandaliwa na Jumuiya ya Watu Wasioona Zanzibar, Awena Hassan Seif amesema (ZANAB) inaiomba Serikali kuongeza uwelewa kwa Jamii kushirikiana na Watu wenye Ulemavu katika kutambua haki na ustawi wao katika mambo mbali mbali ya Kijamii.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.