Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo Ikulu Zanzibar alipozungumza na Balozi wa Norway Nchini Tanzania, Mhe. Tone Tinnes aliyekuja kujitambulisha.
Dkt.Mwinyi amemueleza Balozi, Tinnes kuangalia uwezekano wa kuongeza ushirikiano uliopo baina ya Norway na Tanzania ikiwemo Zanzibar Hasa kusambaza Umeme Vijijini ili kuviendeleza Vijiji hivyo.
Akizungumzia Sekta ya Mafuta na Gesi, Rais Dkt.Mwinyi ameikaribisha Norway kuangalia fursa za uwekezaji kwenye Maeneo hayo na kuongeza ushirikiano kwenye Sekta ya Afya kupitia Hospitali ya Rufaa ya Mnazi Mmoja kwa Wataalamu wa Magonjwa ya Moyo.
Dkt. Mwinyi pia amemueleza Balozi huyo, kuangalia uwezakano wa kuwaendeleza Wakulima wa Mwani wa Zanzibar kupitia Sekta ya Uchumi wa Buluu.
Naye, Balozi Tinnes amemuhakikishia Rais Dk.Mwinyi ushirikiano mzuri uliopo baina ya Ubalozi huo na Shirika la Umeme, Zanzibar (ZECO) kupitia Miradi mbalimbali ya kimkakati ya kukuza huduma za Umeme kwa Visiwa vya Zanzibar.
Kuhusu Sekta ya Afya, Balozi Tinnes alimueleza Rais Dkt.Mwinyi ushirikino uliopo baina ya Hospitali ya Mnazi Mmoja na Hospitali Kuu ya Norway kuwa pande mbili hizo zinashirikiana kubadilishana uzoefu na kusaidiana Wataalamu kwa Maeneo tofauti.