AMEND NA UBALOZI WA USWIS WAMEFANIKIWA KUWEKA MIUNDOMBINU YA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI

INSPEKTA WA JESHI LA POLISI

Katika jitihada za kupunguza Ajali za Barabarani kwa Wanafunzi Nchini Jijini Tanga, Shirika la Amend kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uswis wamefanikiwa kuweka Miundombinu alama za Usalama Barabarani yenye lengo la kuhakikisha Wanafunzi wanavuka salama katika Safari ya kwenda na kurudi Shuleni.

Zoezi la Uwekeji Miundombinu hiyo imefanyika katika Shule ya msingi Makorora na azimio zilizopo katika Jiji la Tanga Mkoani Tanga lijumuisha Ujenzi wa njia za Watembea kwa Miguu, Vivuko 4 vya Pundamilia, Matuta Saba ya kupunguza Mwendo Kasi, alama 15 za Barabarani, na Michoro 16 ya Usalama Barabarani.

Akizungumza katika hafla hiyo mkurugenzi wa shirika la amend Tanzania Simon Kalolo amesema Mradi huo ni Mpango wa kuboresha Miundombinu Salama ya Watembea kwa Miguu ni sehemu ya Mradi wa mwaka mmoja unaoitwa "Usalama wa Pikipiki kwa Vijana Tanzania".

Nae Mwakilishi wa Ubalozi wa Uswisi Rashid Mbaramula amesema Uswis imekuwa ikishiriki kikamilifu katika kufanikisha Miradi ya Maendeleo.
Awali Inspekta wa Jeshi la Polisi Rajab Mhumbi amesema vivuko vya Barabarani amewaomba Wananchi kuilinda Miundombinu hiyo

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.