Habari

TANZANIA KUNUFAIKA NA UANACHAMA KATIKA JUMUIYA ZA NISHATI ZA AFRIKA MASHARIKI

   Tanzania inatarajiwa kunufaika na uanachama wake katika jumuiya za nishati za Afrika Mashariki yaani (East African Power Pool) na Kusini (South Africa Power Pool) katika maeneo mbalimbali ikiwemo biashara ya umeme pamoja na kuunganishwa katika gridi ya pamoja.

DKT.MWINYI ASIFU FURSA ZA BIASHARA BAINA YA ZANZIBAR NA COMORO

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar na Comoro zina Mahusiano maalum ya kuchanganya damu wa kindugu hivyo ameridhia kufunguliwa kwa Konseli Mkuu wa Comoro hapa Zanzibar.

     Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Balozi mpya wa Tanzania katika visiwa vya Comoro Mhe.Saidi Yakubu aliyefika kumuaga baada ya kuteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Ikulu Zanzibar tarehe 14 Mei 2024.

SERIKALI YATAMBUA UMUHIMU WA UTAFITI KATIKA NYANJA MBALIMBALI ZA MAENDELEO

    Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu na mchango wa utafiti wa kisayansi katika nyanja za kijamii, kiuchumi na kisayansi zinazochangia kuchochea maendeleo ya nchi.

CHINA NA TANZANIA KUSHIRIKIANA KATIKA HUDUMA ZA MAKUBUMBUSHO

    Makumbusho ya Taifa ya China na Tanzania zimekubaliana kushirikiana katika kubadilishana uzoefu, teknolojia na kuwa na maonesho ya pamoja kwa lengo la kuhakikisha kuwa huduma za makumbusho zinakuwa na faida kwa pande zote mbili za nchi hizo.

    Makubaliano hayo yamefikiwa katika mazungumzo kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la China, Gazo Zheng yaliyofanyika kwenye Makumbusho ya China jijini Beijing Mei 14,2024.

ZAIDI YA WANANCHI ELFU 40 HALMASHAURI YA MTAMA KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA

   Zaidi ya wananchi Elfu 40 kutoka katika Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi wanatarajiwa kunufaika na mradi wa Maji na usafi wa mazingira unatekelezwa  na taasisi isiyo ya kiserikali ya 'Heart to Heart' chini ya ufadhili wa Shirika la Kimataifa la KOICA utakaoghalimu kiasi cha shilingi Bilioni 1.6

    Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo katibu tawala Mkoa wa Lindi Bi zuwena Omary amewahimiza wananchi na taasisi mbalimbali zilizopo ndani ya Mkoa huo kutunza na kulinda vyanzo vya maji ili viendelee kutoa ya maji kwa  kwa muda mrefu.

DKT MWINYI ASIFU MAFANIKIO YA HATI SAFI ZILIZOWASILISHWA KUPITIA RIPOTI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesifu Mafanikio makubwa ya hati safi zilizowasilishwa kwa Serikali, kufuatia Taarifa ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Zanzibar, (CAG) na kuzitaka Taasisi na Mashirika ya umma zenye hati zilizo na Dosari kujitathmini na kuzifanyia kazi ili mapungufu yasiendelee kujirejea.

Dk. Mwinyi ameyaeleza hayo Ikulu  baada ya kuwasilishwa kwa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Zanzibar, (CAG), dk. Othman Abbas Ali.

SMZ IMEIHAKIKISHIA SERIKALI YA BRAZIL KUONGEZA USHIRIKIANO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameihakikishia Serikali ya brazil ushirikiano mzuri uliopo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa kwenye Miradi mbalimbali ya maendeleo.

Rais Dk. Mwinyi ameyaeleza hayo Ikulu Zanzibar, alipozungumza na Balozi mpya wa Brazil Nchini Tanzania, Mhe. Gustavo Martins Nogueira na ujumbe wake wake aliofika kujitambulisha. 

SMT KUFANYA TATHIMINI YA UHARIBIFU WA BARABARA NA MADARAJA.

Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa amesema Serikali kwa sasa imesitisha Ujenzi wa Barabara mpya mpaka itakapokamilisha kufanya tathimini ya uharibifu wa Barabara na Madaraja uliosababishwa na Mvua zilizonyesha na badala yake kuendelea kurejesha Mawasiliano maeneo yaliyokatika.

WAZIRI MASOUD AMETEMBELEA UJENZI WA SOKO LA MWANAKWEREKWE NA JUMBI.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Mhe Masoud Ali Mohammed ametembelea ujenzi wa  Soko  la  Mwanakwerekwe na  Jumbi ili   kuangali miundo mbinu Rafiki kwa Wafanyabiashara.

Akizungumza katika Ziara hiyo waziri masoud amesema Serikali inafanya juhudi mbali mbali ili kuhakikisha Wafanya Biashara Wanafanya Kazi katika Mazingira bora pamoja na  kuwapa Kipaumbele waliokuwa wakifanya kazi mwanzo katika Masoko hayo .

WASIMAMIZI WA UCHAGUZI KUFUATA MAADILI

Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC inaendesha Mafunzo ya Uchaguzi kwa Waratibu na Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Ngazi ya Jimbo  Kwahani.

Akifungua Mafunzo hayo ya Siku Tatu Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Jacobs Mwambegele amewataka kuzingatia Sheria,Kanuni na Miongozo ya uchaguzi ili kuendesha Uchaguzi kwa haki na kuondoa Malalamiko

Amesema Tume imewateuwa kutokana na sifa za kusimamia ,hivyo wazingatie Mafunzo hayo pamoja na kuwashirikisha Wadau wa uchaguzi kupitia Vyama vyao katika hatua ili kurahisisha utekele,aji wa Majukumu yao

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.