WASIMAMIZI WA UCHAGUZI KUFUATA MAADILI

MH JAJI JACOBS MWAMBEGELE

Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi INEC inaendesha Mafunzo ya Uchaguzi kwa Waratibu na Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Ngazi ya Jimbo  Kwahani.

Akifungua Mafunzo hayo ya Siku Tatu Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Jacobs Mwambegele amewataka kuzingatia Sheria,Kanuni na Miongozo ya uchaguzi ili kuendesha Uchaguzi kwa haki na kuondoa Malalamiko

Amesema Tume imewateuwa kutokana na sifa za kusimamia ,hivyo wazingatie Mafunzo hayo pamoja na kuwashirikisha Wadau wa uchaguzi kupitia Vyama vyao katika hatua ili kurahisisha utekele,aji wa Majukumu yao

Mkurugenzi wa Uchaguzi INEC Ramadhan Kailima amesema Mafunzo hayo yana umuhimu katika kuwajenga Wasimamizi hao ili kutekeleza Majukumu yao kwa uhakika

Jumla ya mada 12 zinazohusiana na Uchaguzi zitawasilishwa katika Mafunzo kwa ajili ya Uchaguzi huo mdogo wa Jimbo la kwahani unaotarajiwa kufanyika June 8 baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kufariki Dunia

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.