WAZIRI MASOUD AMETEMBELEA UJENZI WA SOKO LA MWANAKWEREKWE NA JUMBI.

MH MASOUD ALI MOHAMMED

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Mhe Masoud Ali Mohammed ametembelea ujenzi wa  Soko  la  Mwanakwerekwe na  Jumbi ili   kuangali miundo mbinu Rafiki kwa Wafanyabiashara.

Akizungumza katika Ziara hiyo waziri masoud amesema Serikali inafanya juhudi mbali mbali ili kuhakikisha Wafanya Biashara Wanafanya Kazi katika Mazingira bora pamoja na  kuwapa Kipaumbele waliokuwa wakifanya kazi mwanzo katika Masoko hayo .

Waziri wa Fedha na Mipango Mh Sada Mkuya Salum na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na uchukuzi Dk Khalid Salum Mohammed amesema Serikali imetumia Fedha nyingi ili kuhakikisha Zanzibar  inakuwa na Masoko ya kisasa na kuahidi kuimarisha Miundo Mbinu ya Barabara ili kuwarahisishia  wafanya Biashara katika kazi zao .

Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Khamis Bakari Khamis  ambae ni msimamizi wa Ujenzi wa Masoko hayo  amesema  bado wapo katika  hatua za mwisho ili kukamilisha ujenzi huo na kuwapa nafasi Wananchi kufanya Biashara zao .

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.