Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara maalum za SMZ Mhe Masoud Ali Mohammed ametembelea ujenzi wa Soko la Mwanakwerekwe na Jumbi ili kuangali miundo mbinu Rafiki kwa Wafanyabiashara.
Akizungumza katika Ziara hiyo waziri masoud amesema Serikali inafanya juhudi mbali mbali ili kuhakikisha Wafanya Biashara Wanafanya Kazi katika Mazingira bora pamoja na kuwapa Kipaumbele waliokuwa wakifanya kazi mwanzo katika Masoko hayo .
Waziri wa Fedha na Mipango Mh Sada Mkuya Salum na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na uchukuzi Dk Khalid Salum Mohammed amesema Serikali imetumia Fedha nyingi ili kuhakikisha Zanzibar inakuwa na Masoko ya kisasa na kuahidi kuimarisha Miundo Mbinu ya Barabara ili kuwarahisishia wafanya Biashara katika kazi zao .
Kamishna wa Chuo cha Mafunzo Khamis Bakari Khamis ambae ni msimamizi wa Ujenzi wa Masoko hayo amesema bado wapo katika hatua za mwisho ili kukamilisha ujenzi huo na kuwapa nafasi Wananchi kufanya Biashara zao .