Habari

JESHI LA POLISI KUANZISHA MKAKATI WA KUKOMESHA VIJANA KUTEMBEA NA SILAHA ZA JADI IKIWEMO MAPANGA ILI KUONDOA UHALIFU.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi limeanzisha Mkakati wa  maalum wa kutembelea Nyumba kwa Nyumba na kuhakikisha Vijana hawatembei na Silaha yoyote ya Jadi itakayosababisha kuhatarisha Usalama wa wananchi katika Jamii.

SERIKALI KUUNDA KAMATI MAALUM KUSHUGHULIKIA HOJA ZA CAG KILA MWAKA

     Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itafanyia kazi changamoto zote zilizojitokeza katika ripoti ya CAG na kuunda kamati maalum itakayoshughulikia kasoro za kiutendaji zinazotokana na hoja za CAG kila mwaka.

     Amemtaka Katibu Mkuu Kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said kuunda kamati hiyo.

SERIKALI KUMSOMESHA MTOTO MWENYE UALBINO ALIYEJERUHIWA GEITA

     Kufuatia tukio la kujeruhiwa kwa kijana Kazungu Julius mtoto wa miaka 10 mwenye Ualbino siku 8 zilizopita katika Kitongoji cha Mtakuja, Mamlaka ya Mji Mdogo wa Katoro, Mkoani Geita Serikali imeingilia kati kukemea vikali vitendo hivyo kwa kuhakikisha aliyetekeza tukio hilo anatiwa nguvuni.

NMB YAORODHESHA HATIFUNGANI YA JAMII KATIKA SOKO LA HISA LA LONDON

     Benki ya NMB imetanua wigo wa kushiriki katika masoko ya mitaji kimataifa kwa kuiorodhesha hatifungani yake ya jamii (NMB Jamii Bond) jana katika Soko la Hisa la London (LSE).

     Hatua hiyo inaifanya NMB kuwa taasisi ya kwanza Tanzania kuwa na hatifungani katika soko hilo kubwa kuliko yote ya hisa duniani na benki ya kwanza Afrika Mashariki, Kati na Kusini kuorodhesha hatifungani ya uendelevu LSE.

KAMISHENI YA UTALII ZANZIBAR NA TAASISI YA UTALII YA JEJU ZASAINI HATI YA USHIRIKIANO KATIKA KUKUZA UTALII

     Kamisheni ya Utalii Zanzibar (ZTC) na Taasisi ya Utalii ya Jeju (JTO) leo zimesaini Hati ya Maridhiano (MoU) ya kushirikiana katika kukuza utalii katika hafla fupi iliyofanyika katika kisiwa cha Jeju, nchini Korea Kusini.

     Hati hiyo imesainiwa na Bi. Hafsa Mbamba, Katibu Mtendaji wa ZTC na Bwana Koh Seung Chul, Afisa Mtendaji Mkuu wa JTO, na kushuhudiwa na Mheshimiwa Mudrik R.Soraga, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.

MAAFISA MANUNUZI WATAKIWA KUJIEPUSHA NA RUSHWA

    Jaji Dhamana wa Mahakama kuu Zanzibar,Kisiwani Pemba,Salim Hassan Bakari amewataka Maafisa Manunuzi,na Wahasibu kuwa waadilifu kwa kutojihusisha na Rushwa na badala yake kusimama imara katika kupiga vita vitendo hivyo kwenye  utekelezaji wa majukumu yao.

    Jaji Dhama ametoa  kauli hiyo wakati akizungumza na Maafisa Manunuzi Wahasibu na Wanasheria katika hafla ya ufungaji wa Mafunzo ya Sheria za Manunuzi huko makatiba kuu ya Chake Chake.

WAKAAZI WA MAGOMENI WAIOMBA SERIKALI KUKAMILISHIWA UJENZI WA MITARO

     Wakaazi wa Jimbo la Magomeni wameomba kukamilishiwa Ujenzi wa Mitaro katika Maeneo yao pamoja na kuimarishiwa Miundombinu ya Maji ili kuwaondoshea kero Wananchi.

    Wakaazi wa Jimbo hilo wakizungumza wakati Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Kichama Talib Ali Talib akiendelea na Ziara zake za kusikiliza kero za Wananchi, wamesema wamekuwa wakipata adha ya Nyumba zao kuingia maji wakati wa Mvua kutokana na kukosekana Mitaro pamoja na shida ya Maji.

WATOTO WATAKIWA KUPATIWA ELIMU BILA KUJALI JINSIA ZAO

     Shirika la Korea khfi linalosimamia Mradi wa kutengeneza Mazingira Rafiki kwa Mtoto wa Kike kuweza kumaliza masomo yake, limewataka Wazazi kuangalia umuhimu wa kuwapatia elimu Watoto bila kujali jinsi zao.

     Akizungumza na Wazazi wa Wanafunzi wa Skuli ya Mtule waliopatiwa Mafunzo ya Siku Nane ya Elimu ya Jinsia, Meneja Miradi wa khfi, Taewan Park, amesema elimu ya jinsia ni msingi wa kujenga Jamii jumuishi kwa Wanawake na Wanaume.

ZANROD KUJENGA MTARO WA KUPITISHIA MAJI YA MVUA KUMVUNI PUJINI

   Wakala wa Barabara Zanzibar Ofisi ya Pemba, imetekeleza agizo la Viongozi Wakuu wa Kitaifa, la Kujenga Mtaro wa kupitishia maji ya Mvua eneo la Kumvuni Pujini.

     Hayo yameelezwa na Injinia Said Rashdi Said kutoka Wakala wa Barabara Pemba, wakati wa Ukaguzi wa Mtaro huo ambao ulikua ni kilio kikubwa kwa Wananchi wa Eneo hilo.

     Amesema lengo la Wakala ni kutatua Kero mbali mbali za Wananchi,na tayari juhudi hizo zimechukuliwa kwa Vitendo na baada ya Mwezi Mmoja ujao Mtaro huo utakua umeshakamilika.

SERIKALI KUSHIRIANA NA TAASISI ZA DINI KATIKA KUSAIDIA HUDUMA ZA KIJAMII

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa Taasisi za Dini kufanya shughuli zao kwa Uhuru na kushirikiana kutoa huduma kwa Jamii na kutatua matatizo yao.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.