SMZ IMEIHAKIKISHIA SERIKALI YA BRAZIL KUONGEZA USHIRIKIANO

RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi ameihakikishia Serikali ya brazil ushirikiano mzuri uliopo na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa kwenye Miradi mbalimbali ya maendeleo.

Rais Dk. Mwinyi ameyaeleza hayo Ikulu Zanzibar, alipozungumza na Balozi mpya wa Brazil Nchini Tanzania, Mhe. Gustavo Martins Nogueira na ujumbe wake wake aliofika kujitambulisha. 

Katika mazungumzo yao wamegusia kuendeleza Uhusiano uliopo baina ya Zanzibar na Brazil kwenye Nyanja mbalimbali za Miradi ya maendeleo ikiwemo Sekta ya Afya, Miundombinu ya Barabara, Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba, kuimarisha ushirikiano Wa biashara, Utalii pamoja na fursa za uwekezaji kwenye Sekta ya Mafuta na Gesi Zanzibar.

Dk. Mwinyi amesema Serikali itadumisha Ushirikiano wake na Brazili hususan kwenye Biashara ya Sukari na Mchele ili kupungumza mfumko wa Bei za Bidhaa hizo Nchini.

Akizungumzia Sekta ya Afya Rais Dk. Mwinyi amemweleza Balozi huyo nia ya Serikali kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo baina yake na Brazili pia kudumisha na kuendelea kutoa ushirikiano kwa Timu ya Madaktari wa Brazil wanaokuja Zanzibar kwa nia ya kuendeleza ushirikiano wao kwenye Sekta ya Afya .     

Balozi Nogueira amemueleza Rais Dk. Mwinyi ushirikiano wa pande hizo mbili za Diplomasia na kwamba Serikali ya Brazil itaelekeza nguvu zake zaidi kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hasa kwenye eneo la Afya ya uzazi.

Kuhusu Ushirikiano wa Biashara Balozi Nogueira pia amemweleza Rais Dk. Mwinyi kwamba Brazili ni msalishaji mkubwa wa Sukari Duniani hivyo aliitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kushirikiana zaidi kwenye eneo hilo kwa Watu wa pande mbili hizo kunufaika na Biashara ya Sukari.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.