DKT MWINYI ASIFU MAFANIKIO YA HATI SAFI ZILIZOWASILISHWA KUPITIA RIPOTI

RAIS WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesifu Mafanikio makubwa ya hati safi zilizowasilishwa kwa Serikali, kufuatia Taarifa ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Zanzibar, (CAG) na kuzitaka Taasisi na Mashirika ya umma zenye hati zilizo na Dosari kujitathmini na kuzifanyia kazi ili mapungufu yasiendelee kujirejea.

Dk. Mwinyi ameyaeleza hayo Ikulu  baada ya kuwasilishwa kwa Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali Zanzibar, (CAG), dk. Othman Abbas Ali.

Amesema, pamoja na mapungufu na matatizo yanayohitaji kushughulikiwa kwa kuchukuliwa hatua mbalimbali ili kufanya vizuri zaidi Siku za usoni ,hivyo amemuagiza Katibu Mkuu kiongozi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi, Mhandisi Zena Ahmeid Said kuunda kamati maalumu itakayoshughulikia kasoro hizo ili kuzifanyia Kazi.

Dk. Mwinyi, amezionya baadhi ya Taasisi za Serikali kuingia kwenye Mikataba ya utekelezaji wa Miradi ya Serikali bila kuishirikisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali jambo ambalo ni kosa Kisheria.

Amewataka Viongozi wa Serikali wa ngazi zote, kuendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Zanzibar panapokua na Wajibu wa kufanya hiyo. 

Akiwasilisha Ripoti yake, CAG Dk. Othman Abbas Ali, ameishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa na Mifumo michache itakayodhibiti siri za Serikali pamoja na mapato ya Serikali yasipotee.

Dk. Abass, amesema Ukaguzi huo ulibaini kasoro kwa mashirika na Kampuni hizo kutokuwa na ufanisi wa utoa huduma na hayaendani na malengo na mkakkati yaliyojiwekea kwa ushindani na Taasisi nyengine Binafsi.

 Jumla ya Ripoti nane zilikabidhiwa Serikali ikiwemo ya Serikali kuu (Mawizara na Taasisi zote).

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.