Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa amesema Serikali kwa sasa imesitisha Ujenzi wa Barabara mpya mpaka itakapokamilisha kufanya tathimini ya uharibifu wa Barabara na Madaraja uliosababishwa na Mvua zilizonyesha na badala yake kuendelea kurejesha Mawasiliano maeneo yaliyokatika.
Majaliwa amesema hayo akiwa Ziarani katika halmashauri ya Busokelo Mkoani Mbeya alipokuwa akizindua Jengo la kisasa la Halmashauri hiyo linalokwenda kuongeza ufanisi kwa Watumishi kwa kutoa huduma katika Mazingira rahisi na Wananchi kufurahia huduma.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa halmashauri ya Busokelo Bi loema Peter amesema jengo hilo mpaka kukamilika limetumia gharama Shilingi Bilioni Sita na inahitaji Bilioni 2.4 kukamilisha ujenzi wa Ukumbi na uzio.