FURSA MPYA KWA VIJANA BILIONI 2 KWA WATENGENEZAJI WA MAUDHUI

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda, amesema Wizara imepatiwa kiasi cha TZS bilioni 2 itakayowawezesha watengenezaji wa maudhui mbalimbali mitandaoni kuimarisha kazi zao na kuwaongezea kipato kupitia majukwaa ya kidijitali.

Amesema hayo Januari 29, 2026 jijini Dodoma na kubainisha kuwa, fedha hizo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kuyawezesha makundi yote ya watengeneza maudhui ikiwemo katika Sekta ya Utalii, Michezo, Habari, Jamii, Muziki, Filamu na sanaa nyinginezo.

SHETTA AIWAKILISHA DAR ES SALAAM KATIKA JUKWAA LA UONGOZI WA MAMEYA AFRIKA

Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Nurdin Bilal Juma (Shetta), kwa sasa yupo Cape Town, Afrika Kusini, akishiriki katika mkutano wa African Mayoral Leadership Initiative (AMALI) unaowakutanisha mameya na viongozi wa miji kutoka barani Afrika.

Katika mkutano huo, Mstahiki Meya alipata fursa ya kuwasilisha maono ya urithi wa uongozi (legacy pitch) kwa niaba ya Jiji la Dar es Salaam akiweka mbele ajenda ya maendeleo jumuishi, ajira kwa vijana, na uongozi wa miji unaozingatia watu.

DKT SAMIA AZINDUA MPANGO WA KUSOMA KUANDIKA NA KUHESABU

Rais Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mh.Dk. Samia Suluhu Hassan Amezindua Mpango Mkakati Wa Sayansi Wa Kujenga Umahiri Wa Kusoma, Kuandika Na Kuhesabu (Kkk)Kwa Watoto Wa Elimu Awali Na Wanafunzi Wa Darasa La Kwanza Na La Pili.

Akizungumza Katika Uzinduzi Wa Mpango Huo Uliofanyika Jiji Dar Es Salaam, Rais SamiaAmesema Kuwa Serikali Imejidhadhati Kuhakikisha Kuwa Hakuna Mtoto Atakaye Fika Darasa La Tatu Bila Ya Kuwa Na Uwezo Wa Kusoma Kuandika, Kuandika Na Kuhesabu. 

MFUMO WA KIELEKRONI MAHAKAMANI WARAHISISHA UENDESHAJI WA KESI

Jaji Mkuu Wa Zanzibar, Khamis Ramadhani Abdalla Amesema Kuwepo Kwa Mfumo Wa Uendeshaji Wa Mashauri Kwa Njia Ya Kielektroniki Kumerahisisha Usikilizaji Wa Kesi, Na Kuchangia Upatikanaji Wa Haki Kwa Haraka.

Akizindua Mfumo Wa Majaribio Wa Uendeshaji Wa Mashauri Kwa Njia Ya Kielektroniki Huko Verde Amesema Lengo La Kuanzisha Mfumo Huo Ni Kuongeza Ufanisi Na Uwajibikaji Katika Mahkama Pamoja Na Kuondosha Urasimu Wa Haki Kwa Wananchi.

Subscribe to
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.