Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewataka Washiriki wa Kongamano la Miaka 60 ya Mapinduzi kulitumia Kongamano hilo kujadili na kutoa maoni kwa Serikali kuhusiana na fursa zilizopo katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo.
Akifungua Kongamano la Miaka 60 ya kuenzi Mapinduzi ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohammed Shein Dkt.Mwinyi amesema ni vyema kuhusisha sera na mpango mkuu wa Serikali kupitia vipaumbele vilivyowekwa.
Amesema Makongamano kama hayo husaidia kuongeza uelewa wa masuala muhimu ya Nchi kwa kuwakumbusha walipo na wanapotoka na kushauri umuhimu wa kuimarisha uhusiano huo wa kitaaluma kwa kufanya utafiti utakaosaidia kuleta maendeleo kwa pande zote mbili
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Januari Makamba na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheri na Utawala Bora Mhe.Haroun Ali Suleiman wamesema hatua za maendeleo zilizofikiwa zinakuza fursa za kiuchumi na kuongeza ustawi .
Mkuu wa Chuo cha Utawala wa Umma Ipa Dkt.Shaaban Mwinyichum na Mwenyekiti wa Baraza Uongozi Kituo cha CFR Ramadhan Muombwa Mwinyi amesema Kongamano hilo ni sehemu ya utekelezaji wa Hati ya makubaliano ya kitaaluma kwa kuongeza Wataalamu katika Sekta mbali mbali na kuibua fursa kwa Wananchi.
Kongamano hilo limeandaliwa na Chuo cha Utawala wa Umma Zanzibar Ipa na Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt.Salim Ahmed Salim CFR lilikuwa na kauli mbiu "Mchango wa Diplomasia katika Maendeleo Endelevu ya Uchumi wa Buluu