Timu ya 33 ya Madaktari kutoka China imesema itaendelea kuwapatia Taaluma ya Maradhi mbali mbali Madaktari Wanafunzi wanaosomea Fani ya Udaktari wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA.
Akizungumza baada ya kutoa Mafunzo kwa Madaktari Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA, Dkt Jiao Cheng wa Maradhi ya Masikio Koo ya Pua (ENT) amesema Maradhi hayo yanawasumbua Watu wengi na kuwepo kwa Madaktari wataweza kukabiliana nayo.
Amefahamisha kuwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mnazimmoja wamekuwa wakipokea Wagonjwa wengi wenye matatizo ya Koo Masikio na Pua, dalili ya Awali huwa ni Kukoroma, ambapo Watu wengi huona ni jambo la kawaida hivyo ameshauri wenye tatizo hilo wafike Hospitali kwa ajili ya uchunguzi.
Madaktari Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar SUZA wameshukuru kwa hatua ya Madaktari wa Kichina kuwapatia taaluma hiyo ambayo itawasaidia katika Masomo yao.