JKU SC YAUPIGIA HESABU UBINGWA WA LIGI KUU ZNZ

Katibu Wa Klabu Ya Jku Sc Khatibu Shazil Khatibu Amesema Timu Yao Inaendelea Na Maandalizi Ya Kuhakikisha Mzunguko Wa Pili Wanafanya Vizuri Ili Kubeba Ubingwa

Katibu Shazil Amesema Malengo Ya Jku Ni Kufanya Vizuri Katika Michuwano Ya Ligi Kuu Na Kombe La Fa Huku Akigusia Kuhusu Usajili Waliofanya.

KATIBU NEC ATEMBELEA MIRADI YA AFYA HOSPITALI YA RUFAA KILIMANJARO

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI), Rabia Abdalah, ambaye pia ni mlezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Kilimanjaro, ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro kwa lengo la kujionea utekelezaji wa baadhi ya miradi ya maendeleo inayoendelea katika hospitali hiyo.

ACT WAZALENDO YAIOMBA ZEC KUSIMAMISHA UCHOMAJI NYARAKA ZA UCHAGUZI

Chama cha ACT Wazalendo Zanzibar kimeiomba Tume ya Uchaguzi Zanzibar–ZEC kusimamisha zoezi la uteketezaji wa nyaraka na vifaa vya Uchaguzi kwa kile walichodai ni mpaka mashauri yaliyoko Mahakamani yamalizike.

Kauli hii imekuja kutokana na Tamko la Tume ya Uchaguzi lililotolewa hapo Jana likieleza nia ya Tume kuteketeza nyaraka zote za Uchaguzi wa Mwaka 2025 kwa baada ya Siku 90 kwa mujibu wa Sheria.

Subscribe to
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.