BIDHAA ZILIZOSAFIRISHWA ZANZIBAR KWA MWEZI WA MEI 2024 ZAONGEZEKA

MTAKWIMU

   Bidhaa zilizosafirishwa Zanzibar kwa Mwezi wa Mei 2024 zilikuwa na Thamani ya Shilingi Bilioni 5 Nukta 0 Thamani ambayo imeonekanwa kuongezeka.

   Akiwasilisha Takwimu za Biashara za Kimataifa kwa Mwezi huo Mtakwimu kutoka kitengo cha Takwimu za Biashara na Kodi Ndg.Asia Salum Rashid amesema Kundi la Vyakula na Wanyama hai linaongoza kwa Thamani yote ya usafirishaji wa Bidhaaa ambapo bidhaa zilizosafirishwa kwa Makundi maalumu ni Chakula  Wanyama na aina nyengine za  Bidhaa za Viwandani.

   Stela Ngoma Hassan  ni Mchumi Muandamizi kutoka  Chuo Kikuu cha Taifa  cha Zanzibar  SUZA amesema ni vyema kwa  Wafanyabiashara kuongeza biidi ya kutafuta Soko la Biashara  ndani ya Bara la Afrika ili kupunguza Gharama za  usafirishaji wa Bidhaa  Nje ya Bara la Afrika jambo litakalopelekea   Nchi kuzidi kukua Kiuchumu.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.