Bidhaa zilizosafirishwa Zanzibar kwa Mwezi wa Mei 2024 zilikuwa na Thamani ya Shilingi Bilioni 5 Nukta 0 Thamani ambayo imeonekanwa kuongezeka.
Akiwasilisha Takwimu za Biashara za Kimataifa kwa Mwezi huo Mtakwimu kutoka kitengo cha Takwimu za Biashara na Kodi Ndg.Asia Salum Rashid amesema Kundi la Vyakula na Wanyama hai linaongoza kwa Thamani yote ya usafirishaji wa Bidhaaa ambapo bidhaa zilizosafirishwa kwa Makundi maalumu ni Chakula Wanyama na aina nyengine za Bidhaa za Viwandani.
Stela Ngoma Hassan ni Mchumi Muandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA amesema ni vyema kwa Wafanyabiashara kuongeza biidi ya kutafuta Soko la Biashara ndani ya Bara la Afrika ili kupunguza Gharama za usafirishaji wa Bidhaa Nje ya Bara la Afrika jambo litakalopelekea Nchi kuzidi kukua Kiuchumu.