Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohamed Said Mohamed Dimwa amewataka Wananchi kuwasilisha matatizo yao wanayokumbana nayo wapokwenda katika Taasisi za Serikali kufuata huduma ili kuona yanapatiwa ufumbuzi.
Akizungumza katika Ziara Maalum ya Sekretariet ya Kamati Maalum ya Halmashuri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar ya kukagua utendaji kazi wa Viongozi wa Chama na kusikiliza kero za Wananchi katika Wilaya ya Mfenesini Kichama ,amesema CCM ina jukumu la kutatua matatizo mbalimbali katika Jamii ikiwa na lengo la utekelezaji wa ilani ya Chama ili kuepusha usumbufu unaojitokeza hivyo hatua hiyo itawawezesha Wananchi kupata huduma kwa wakati.
Kwa upande wa Wananchi wamesema hatua hiyo itasaidia kuendeleza umoja kati ya Chama na Wananchi na kukiletea ushindi Chama cha Mapinduzi katika Uchaguzi ujao.