DKT. MWINYI ATAKA WAJANE WANAHITAJI KUTAMBULIWA KISHERIA

JUMUIYA YA WAJANE

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Wajane wanahitaji kutambuliwa rasmi kisheria, kuheshimiwa, kuwezeshwa kiuchumi na huduma bora za afya.

   kifungua Mkutano wa Kwanza wa Wajane Afrika Dk.Mwinyi amesema hatua hiyo italeta matumaini kwa Watu hao na kuweza kujikimu kimaisha pamoja na kuwajengea thamani ndani ya Jamii.

   Dkt.Mwinyi ameleeza kuwa Mkutano huo utumike kwa kubadilishana mawazo na uzoefu kwa lengo la kujenga muelekeo wa baadae wa nafasi ya Wajane katika Bara la Afrika.

    Aidha amewasisitiza Washiriki wa Mkutano huo kutembelea vivutio mbalimbali vya Utalii na Uwekezaji Zanzibar ili kusaidia ukuwaji wa Uchumi pamoja na kujionea maendeleo yaliyofikiwa.

    Waziri wa maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe Riziki Pembe Juma amesema  wataendelea, kuwasimamia Wajane na kuwaunganisha  katika mambo ya maendeleo kwa kuanzisha Majukwaa katika ngazi za Shehia, Wilaya, Mkoa hadi Taifa   ili kutoka fursa za kiuchumi pamoja na kujadili masuala yote yanayowahusu Wajane wote wa Tanzania na Afrika kwa ujumla . 

   Baadhi ya Wake wa Viongozi na Viongozi wa Taasisi za Wajane Afrika waliohudhuria Mkutano huo wakaeleza baadhi ya mambo wanayoyapitia Wajane na kuyatafutia njia za ufumbuzi.

recommended
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.