TAASISI YA SAZANI TRUST YAONESHA UMUHIMU WA ZIARA ZA KIMASOMO KWA WANAFUNZI

SAZANI TRUST

    Ziara za Kimasomo kwa Wanafunzi imetajwa kuwa ni njia mojawapo ya kuwaongezea uelewa kwa baadhi ya mambo ambayo Wanafundishwa Darasani.

     Mkurugenzi Mtendaji Sazani Trust, Ndg.Safia Mkubwa Abdalla, ameeleza hayo huko Dole, katika Maonyesho ya Nanenane, amesema Elimu inayopatikana kupitia Ziara za Kimasomo zinawawezesha Wanafunzi kujua asili ya baadhi ya Vitu ambavyo wamekua wakivitumia wakiwa Masomo yao.

      Ndg.Abdalla Ali Said Mwalim kutoka Skuli ya Mtoni amesema miongoni mwa taaluma wanayowapa Wanafunzi ni umuhimu wa kuhifadhi Mazingira na kutambua mbinu mbalimbali za kutumia baadhi ya Taka kwenye matumizi mengine.

     Ziara hiyo ya Siku Moja ilioandaliwa na Sazani Trust, imeshirikisha Wanafunzi kutoka Skuli mbalimbali ikiwemo Lumumba, Hurumzi na Kibweni na kutembelea Mashamba ya Viungo Kizimbani na Maonyesho ya Nanenane Dole.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.