Habari

SHIRIKA LA ZSTC LIMETAKIWA KUSHIRIKINA NA WAKULIMA WA ZAO LA KARAFUU KWA KUINGIA NAO MIKATABA NA KUWAPA NYENZO HASA KATIKA MASHAMBA YA SERIKALI

Dkt Samia Ameyasema Hayo Huko Madungu  Katika Hafla Ya Ufunguzi Wa Jengo La Uwekezaji La Shirika La ZSTC Ikiwa Ni Katika Shamra Shamra  Za Miaka 6o Ya Mapinduzi Ya Zanzibar   Na Kusema    Hatua Hiyo Itasaidia Kuzalisha Karafuu Kwa Kiwango Kikubwa Ili Kukidhi Mahitaji Ya Soko La Dunia. 

SERIKALI INA KILA SABABU YA KUFANYA MABADILIKO KATIKA SEKTA YA BAHARINI ILI KUWEKA MAZINGIRA MAZURI YA USAFIRI WA BAHARI

Ameyaeleza hayo Rais Wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Ambae Ameshuhudia Utiaji Saini Mkataba Wa Ujenzi Wa Bandari Ya Maruhubi Ikulu Zanzibar, Amesema Serikali Imeamua Kujenga Bandari Ya Maruhubi Kutokana Na Bandari Ya Malindi Kuzidiwa Na Abiria Pamoja Na Mizigo Na Kusababisha Msongamano.

Amesema Mradi Huo Utakuwa Mfano Mkubwa Wa Ushirikiano Wa Sera Ya Serikali Na Sekta Binafsi Ya PPP Katika Kufikia Malengo Ya Utekelezaji Wa Miradi Mbalimbali Nchini.

SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA UJENZI WA MAJENGO YA KISASA YA SKULI ZA GHAROFA ILI KUONA WATOTO WANASOMA KATIKA MAZINGIRA BORA.

Dk.Mwinyi Ameyasema Hayo Wakati Akifungua Skuli Ya Sekondari Mwembeladu Iliyopewa Jina La Skuli Ya Tumekuja Ikiwa Ni Shamrashamra Za Kuadhimisha Miaka 60 Ya Mapinduzi Ya Zanzibar, Amesema Ni Vyema Kuimarisha Sekta Hiyo Ili Kuona Wanafunzi Wanaondokana Na Kuingia Kwa Mikondo Miwili Na Badala Yake Waingie Mara Moja Tu Kwa Siku.

 

Amesema Wizara Inahitaji Madarasa Elfu Tano Jambo Litakalowasaidia Wanafunzi Na Mpaka Sasa Imefikisha Madarasa Elfu Tatu Ambapo Mengine Yanaendelea Kuengezwa Ili Ifikie Idadi Ya Madarasa Elfu Tano.

KIKOSI CHA VALANTIA KIMETAKIWA KUZUNGUSHA UKUTA KATIKA ENEO LA KAMBI YA MWANYANYA, ILI KUIWEKA KATIKA MAZINGIRA SALAMA

Agizo Hilo Limetolewa Na Waziri Wa Fedha Na Mipango Dkt.  Saada Mkuya, Wakati Akizindua Nyumba Tatu Za Kulala Askari Pamoja Na Ofisi Zoni Ya Mjini, Amesema Majengo Hayo Mapya Yanahitaji Kutunzwa Ili Kuimarisha Shughuli Za Kiutendaji Kwa Maafisa Na Askari Wa Kikosi Hicho.

TUME YA UTUMISHI WA MAHKAMA INASAIDIA KUIMARISHA MABADILIKO KATIKA NIDHAMU NA MAADILI KWA WATUMISHI

 

  Ameyasema Hayo Jaji Mkuu Wa Zanzibar Mh Khamis Ramadhan Abdalla Katika Hafla Ya Kuwaapisha Mwenyekiti Na Wajumbe Wapya Wa Tume Ya Utumishi Wa Mahkama Huko Tunguu Mkoa Wa Kusini Unguja.

Jaji Khamisi Ameihimiza  Tume Hiyo Kusimami Upatikanaji Wa Maslahi Ya Wafanyakazi  Na  Ufanisi Na Utendaji.

 

 Mwenyekiti Wa Tume Ya Utumishi Wa Mahkama Jaji Aziza Iddi Suwed Ameahidi Kutumia Maarifa  Katika Kuimarisha  Mahkama.

Hafla Hiyo Imehudhuriwa Na Jaji Kiongozi Wa Mahkama Ya Tanzania Na Viongozi Wengine.

SERIKALI INAPATA MICHANGO MIKUBWA KWA TAASISI YA JANE GOODALL HASA KATIKA TECHNOLOGIA YA KUHIFADHI MISITU NA MALIASILI.

Akizungumza Katika Kongamano La  Tatu La Roots Shoots La Kimataifa Barani Afrika  Katibu Mkuu Wa Wizara Ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili Na Mifugo  Seif Shaban Mwinyi  Amesema Kwa Kutumia Technologia Ya Kuhifadhi Misitu Na Maliasili Vijana Wengi Wamenufaika  Hali Ambayo Inasaidia Kuhifadhi Rasilimali Za Nchi

Amesema Serikali  Itaendelea Kuunga Mkono Juhudi Za Taasisi Hiyo Ili Kuhakikisha Mashirikiano Hayo Yanaimarika.

UWEKEZAJI WA MIRADI YA NYUMBA ZA MAKAAZI KWA WAGENI, UMEKUWA NI WA PILI KWA KULETA MITAJI MIKUBWA HAPA NCHINI.

Ameyasema hayo Makamo Wa Kwanza Wa Rais Wa Zanzibar Othman Masoud Othman, Katika Uzinduzi Wa Mradi Wa Nyumba CPS The Soul Huko Paje, Amesema Hatua Hiyo Itasaidia Kuitangaza Zanzibar Na Kushajihisha Wageni Kuingia Nchini Na Kutembelea Vivutio Vilivyomo.

Amesema Uwekezaji Huo Unaochukuwa Nafasi Ya Pili Badala Ya Hoteli Za Kitalii Utawahakikishia Hifadhi Za Malazi Na Usalama , Ambapo Serikali Inaendelea

Kuimarisha Sera Na Sheria Ili Kutanua Zaidi Shughuli Za Uwekezaji.

VIONGOZI WA JUMUIYA YA WAVUVI YA KIWANI (JUWAKI), WAMEMETAKIWA KUVITUMIA KWA MALENGO YALIYOPANGWA VIFAA PAMOJA NA BOTI ZA UVUVI WALIVYOPATIWA NA BENKI YA NMB.

Hayo yameelezwa na Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman kwenye uzinduzi wa Mkopo Maalumu Wa Boti Yaani (Master Boat), Uliotolewa Na Bank Ya NMB Kwa Jumuiya Ya Wavuvi Wa Kiwani Pemba Amesema Kuwa Boti Hizo Za Kisasa Zitasaidia Kutoa Ajira Kwa Wananchi Wa Kiwani Na Vitongoji Vyake Pamoja Na Kukuza Ipato Vyao.

UCHUMI WA NCHI YOYOTE DUNIANI HAUWEZI KUJENGWA NA SEKTA YA UMMA PEKEE BALI NI LAZIMA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amesema uchumi wa Nchi yoyote Duniani hauwezi kujengwa na Sekta ya umma pekee bali ni lazima kushirikiana na Sekta Binafsi katika uwekezaji wa Miradi mbali mbali ya Kiuchumi.

DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AMEELEZEA KURIDHISHWA NA VIWANGO VYA UJENZI WA BARABARA YA UWANJA WA NDEGE-MNAZIMMOJA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi dkt. Hussein Ali Mwinyi ameelezea kuridhishwa na viwango vya ujenzi wa Barabara ya Uwanja wa Ndege-Mnazimmoja amesema kuwa itakuwa ya mfano na inaendana na kasi ya ukuaji uchumi wa Zanzibar.

Dkt. Mwinyi akizungumza katika uwekaji Jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Bara Bara hiyo   yenye urefu wa Kilomita 6 nukta 8, amesema Serikali lengo la Serikali ni kuona Barabara zote zinajengwa kwa kiwango bora ili zitumike kwa muda mrefu huku akiwataka Wanachi kuacha kufanya Biashara pembezoni mwa Barabara.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.