Hayo yameelezwa na Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar, Mhe. Hemed Suleiman kwenye uzinduzi wa Mkopo Maalumu Wa Boti Yaani (Master Boat), Uliotolewa Na Bank Ya NMB Kwa Jumuiya Ya Wavuvi Wa Kiwani Pemba Amesema Kuwa Boti Hizo Za Kisasa Zitasaidia Kutoa Ajira Kwa Wananchi Wa Kiwani Na Vitongoji Vyake Pamoja Na Kukuza Ipato Vyao.
Waziri Wa Uchumi Wa Buluu Na Uvuvi Mhe. Suleiman Massoud Makame Amesema Kijiji Cha Kiwani Ni Miongoni Mwa Eneo Linalozalisha Mwani Kwa Wingi Kwa Mkoa Wa Kusini Pemba, Kutokana Na Hamasa Inayotolewa Kwa Wakulima Katika Kulipa Thamani Zao Hilo Huku Akiishukuru NMB Kwa Hatua Hiyo.
Mwenyekiti Wa Jumuiya Ya Wavuvi Wa Kiwani Kassim Omar Suleiman Ameishukuru Serikali Kwa Kuendelea Kuwajali Wavuvi Na Wakulima Wa Mwani Kwa Kuwawekea Mazingira Wezeshi Ya Kufanyia Kazi.