Habari

SERIKALI ITAENDELEA KUTOA KIPAUMBELE KWA WATU WENYE ULEMAVU KWA KUWAWEKEA MAZINGIRA RAFIKI YA KIJIFUNZA

Serikali itaendelea kutoa kipaumbele kwa Watu wenye Ulemavu  kwa kuwawekea mazingira rafiki ya kijifunza na kuhakikisha kuwa kundi hilo haliachwi nyuma katika mipango ya Serikali.

Makamu wa Pili wa Rais Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akiwa katika muendelezo wa shamrashamra za miaka 60 ya Mapinduzi,amezunguza na Wananchi wa Pujini Wilaya ya ChakeChake katika ufunguzi wa kituo cha elimu mjumuisho, ambapo amesema Zanzibar inatekeleza mipango ya Kitaifa na Kimataifa kuhakikisha Skuli na Majengo yote yanazingatia mahitaji ya watu wenye Ulemavu.

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR IMEWATAKA WANANCHI KUENDELEA KUITUNZA MIUNDOMBINU INAYOJENGWA IKIWEMO YA SKULI

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imewataka Wananchi kuendelea kuitunza Miundombinu inayojengwa ikiwemo ya Skuli ili kufikia malengo ya Mapinduzi ya mwaka 1964 ya kutoa elimu bure kwa Wazanzibari katika mazingira yaliyo bora zaidi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdullah ameyasema hayo alipoweka Jiwe la msingi katika ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Kiwani ikiwa ni muendelezo wa shamra shamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

JAMBO LA FARAJA NI KUONA KINAMAMA WA BIASHARA YA CHAKULA, WAMEEKEWA MAZINGIRA BORA

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe Tabia Maulid Mwita, amesema ni jambo la faraja kuona Kinamama wa Biashara ya Chakula, wameekewa mazingira bora ya kuendesha biashara zao katika hali ya salama.

Akizindua Soko la Mama Lishe Kinyasini, amesema ujenzi wa Soko hilo ni utekelezaji wa ahadi za Rais Dk Hussein Mwinyi, kwa Wajasiriamali na itakuwa imeshatatua kasoro zilizokuwa zikikwamisha uendeshaji wa biashara zao kwa ufanisi.

WAKATI UMEFIKA KWA VIJANA KUJIFUNZA KUTOKA KWA WAZEE ILI KUWA WAZALENDO WA NCHI YAO

Naibu Waziri Mkuu na Waziri  wa Nishati Mhe Doto Biteko amesema wakati umefika kwa Vijana kujifunza kutoka kwa Wazee ili kuwa Wazalendo wa Nchi yao.

Akizungumza katika Kongamano la kuadhimisha Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Biteko amesema ni vyema kwa Vijana hao kuwa Mstari wa mbele katika kufanikisha maendeleo yao na Taifa kwa ujumla. 

Amesema  kuna baadhi ya Watu ambao Siasa zao ni za ushindani zinazosababisha kufanywa  uzungumzwe kwa mtazamo  tofauti hivyo kutokubali kuvyunjwa Moyo na kusonga mbele Kimaaendeleo. 

MABADILIKO MAKUBWA YA KIUTENDAJI KWA MAMLAKA YA KUKUZA UWEKEZAJI ZANZIBAR (ZIPA), YAMESAIDIA KUONGEZEKA KWA MIRADI MIKUBWA NCHINI.

Akizungumza katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa Hoteli ya Zanzibar Crown Resort, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema hatua hiyo itasaidia kukuza uchumi unaotokana na miradi hiyo kutokana na mahitaji ya Dunia, kubadilika na kufanya kazi kisasa mamlaka hiyo imekuwa ikiharakisha utowaji huduma na kuziomba Taasisi nyengine kujifunza kutoka kwao.

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR INAENDELEA NA AZMA YAKE YA KUIFUNGUA PEMBA KIUCHUMI KWA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA BANDARI YA MKOANI, UJENZI WA BANDARI YA SHUMBA MJINI PAMOJA NA KUIJENGA UPYA BANDARI YA WETE KWA LENGO LA KUWATATULIA WANANCHI TATIZO LA US

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Hemed Suleiman Abdulla, ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa marekebisho ya Bandari ya Mkoani na maegesho ya makontena ikiwa ni mwendelezo wa shamra shamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

KAZI YA UHAKIKI INAFANYIKA KWA UFANISI LICHA YA KUWEPO KWA ONGEZEKO LA IDADI YA WASTAAFU MWAKA HUU.

Akizungumza katika zoezi la uhakiki wa Wastaafu wanaolipwa Pencheni zao na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), linalofanyika kituo cha Kitogani kwa siku mbili, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano  kutoka ZSSF, Raya Hamdani amesema hadi sasa kiasi ya wastaafu elfu tisa wameshafanyiwa uhakiki kati ya wastaafu elfu 13 na mia tano  wanaowatarajia kuwafanyia uhakiki huo, huku akiwaomba wastaafu wote ambao hawatohakikiwa katika kipindi hiki kufuata huduma hiyo makao makuu ili kuepuka usumbufu.

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IMEKUSUDIA KULETA MAPINDUZI KATIKA SEKTA YA ELIMU ILI KUENDANA NA FIKRA NA FALSAFA ZA WAASISI WA MAPINDUZI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla, ameyasema hayo alipoweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Skuli ya Sekondari Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba ikiwa ni shamra shamra ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema lengo la Serikali ni kutatua tatizo la nafasi katika Skuli za maandalizi, Msingi na Sekondari ikiwa ni pamoja na kuwapunguzia Watoto kutembea masafa marefu kutafuta huduma ya Elimu.

WANAWAKE WAMETAKIWA KUA MSTARI WA MBELE KUTANGAZA MAENDELEO YANAYOTEKELEZWA NA SERIKALI.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti Mstaafu wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT, Sophia Simba kwenye kongamano la wanawake wa UWT Taifa la kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Sophia amesema, ni wakati wa Wanawake sasa kundi hilo likawa kinara katika kunadi maendeleo yaliyofikiwa pamoja na kupanga mikakati kwa ajili ya uchaguzi Mkuu mwakani.

Katibu Mkuu wa UWT, Jokate Mwigelo na Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar, Tunu Juma Kondo wamewasisitiza wanawake kushirikiana ili kuiimarisha Jumuiya pamoja na Chama.

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA IMEANZA KUSIKILIZA MAONI YA WADAU YA MISWADA MINNE YA SHERIA

Akitoa taarifa kuhusu mwenendo wa zoezi hilo Bungeni Jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria,Mhe. Dk. Joseph Mhagama amewataka Watanzania kuendelea kujitokeza kutoa maoni yao katika miswada hiyo.

Baadhi ya Washiriki wa Kikao hicho wakiwemo Viongozi wa Vyama vya Siasa wametoa ushauri wao kuhusu miswada hiyo, akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu, Japhet Maganga na Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Mhe. Zitto kabwe.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.