Dk.Mwinyi Ameyasema Hayo Wakati Akifungua Skuli Ya Sekondari Mwembeladu Iliyopewa Jina La Skuli Ya Tumekuja Ikiwa Ni Shamrashamra Za Kuadhimisha Miaka 60 Ya Mapinduzi Ya Zanzibar, Amesema Ni Vyema Kuimarisha Sekta Hiyo Ili Kuona Wanafunzi Wanaondokana Na Kuingia Kwa Mikondo Miwili Na Badala Yake Waingie Mara Moja Tu Kwa Siku.
Amesema Wizara Inahitaji Madarasa Elfu Tano Jambo Litakalowasaidia Wanafunzi Na Mpaka Sasa Imefikisha Madarasa Elfu Tatu Ambapo Mengine Yanaendelea Kuengezwa Ili Ifikie Idadi Ya Madarasa Elfu Tano.
Dk. Mwinyi Katika Ufunguzi Huo Amewapongeza Walimu Kwa Jitihada Wanazozichukua Katika Kutoa Elimu Bora Kwa Wanafunzi Na Kwenda Na Mageuzi Ya Serikali Katika Sekta Hiyo Na Kuahidi Serikali Itahakikisha Inaendelea Kuimarisha Mazingira Bora Na Maslahi Yao.
Waziri Wa Elimu Na Mafunzo Ya Amali Zanzibar, Mhe Lela Mohamed Mussa, Amempongeza Rais Mwinyi Kwa Maendeleo Anayoleta Kwa Wananchi Wa Zanzibar, Ikiwemo Sekta Ya Elimu Hatua Hiyo Inaonesha Kutekeleza Kwa Vitendo Ikiwemo Kujenga Skuli Za Ghorofa Unguja Na Pemba Ili Sekta Ya Elimu Iweze Kuleta Maendeleo, Hasa Kuelekea Kipindi Hiki Cha Kutimiza Miaka 60 Ya Mapinduzi Ya Zanzibar.
Akitoa Maelezo Ya Kitaalamu Ya Ujenzi Wa Skuli Hiyo, Katibu Mkuu Wa Wizara Hiyo Khamis Abdalla, Amesema Skuli Hiyo Imejengwa Na Kampuni Ya Crje East Afrika Limited Na Kusimamiwa Na Mshauri Elekezi Kampuni Ya Milinium Coslated Group Kwa Gharama Ya Shilingi Bilioni 4 Nukta 48 Ambapo Fedha Hizo Zimetolewa Na Muwekezaji Aliyekabidhiwa Kuendeleza Jengo Lilokuwa Skuli Ya Tumekuja.
Skuli Hiyo Ya Kisasa Ina Uwezo Wa Kuchukua Wanafunzi Zaidi Ya Elfu Moja Kwa Uwiano Wa Wastani Wa Wanafunzi Aroubaini Na Tano Kwa Kila Darasa Kwa Mkondo Mmoja Na Ndio Msingi Mkuu Wa Maendeleo Nchini.