VIONGOZI WANADHAMIRA NJEMA YA KULETA MAENDELEO ENDELEVU YATAKAYO INUA HALI ZA UCHUMI KWA WANANCHI

Dkt. Mwinyi akizungumza katika shamra shamra za kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 katika mazoezi yaliyoanzia mnara wa muembe kisonge hadi uwanja wa amani, amesema Serikali imeamua kuimarisha viwanja vya michezo ili kufanyika michezo mbali mbali huku akiisisitiza jamii kushiriki katika vikundi vya mazoezi ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.


Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema Serikali itaendelea kuimarisha sekta ya michezo hatua kwa hatua.

SERIKALI INAENDELEA KUWEKEZA KWENYE MIUNDOMBINU YA SEKTA YA ELIMU

Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inaendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya sekta ya elimu ili kuwawezesha vijana kusoma fani tofauti ndani ya Nchi.

 Rais wa Zanzibar ameyasema hayo katika mahafali ya 19 ya Chuo kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA na kuwatunuku vyeti, stashahada, shahada, shahada za uzamili na uzamivu kwa wahitimu wa Chuo hicho kwa mwaka wa masomo 2022/2023, huko Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja.

Subscribe to Dkt. Mwinyi
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.