Akizungumza Katika Kongamano La Tatu La Roots Shoots La Kimataifa Barani Afrika Katibu Mkuu Wa Wizara Ya Kilimo Umwagiliaji Maliasili Na Mifugo Seif Shaban Mwinyi Amesema Kwa Kutumia Technologia Ya Kuhifadhi Misitu Na Maliasili Vijana Wengi Wamenufaika Hali Ambayo Inasaidia Kuhifadhi Rasilimali Za Nchi
Amesema Serikali Itaendelea Kuunga Mkono Juhudi Za Taasisi Hiyo Ili Kuhakikisha Mashirikiano Hayo Yanaimarika.
Mkurugenzi Mtendaji Wa Taasisi Ya Jane Goodall Tanzania Frederic Kimaro Amesema Taasisi Hiyo Inatoa Kipaumbele Katika Kuwapa Mafunzo Vijana Dhidi Ya Kulinda Viumbe Vya Porini Pamoja Na Kufanya Utafiti Wa Elimu Ya Mazingira Na Viumbe Na Ameahidi Kuendeleza Ushirikiano Na Serikali Katika Kutunza Misitu.
Kongamano Hilo La Kimataifa Limehudhuriwa Na Wawakilishi Wa Nchi Tofauti Ikiwemo Tanzania, DRC, Afrika Ya Kusini Na Taasisi Za Elimu Ya Juu.