Habari

ZANZIBAR INAADHIMISHA MIAKA 60 YA MAPINDUZI IKIWA IMEPIGA HATUA KUBWA KATIKA KUTEKELEZA MIRADI SEKTA YA ELIMU.

Ameyasema hayo Makamu Wa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dk Philip Isdor Mpango wakati wa uzinduzi wa   Skuli Ya  Elimu  Mjumuisho-Jendele   Dk Mpango Amesema  Mapinduzi Ya Zanzibar Yameiletea Heshima Kubwa Zanzibar Ambapo Sekta Ya Elimu Imepewa Umuhimu Na Kuweka Usawa Katika Upatikanaji Wa Elimu Ikiwemo Mjumuisho

ULINZI UNAHITAJIKA KATIKA MIUNDOMBINU YA MAJI

Rais Mstahafu Wa Awamu Ya Nne Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Amesema Serikali Inafanya Juhudi Kubwa Katika Kuleta Maendeleo Na  Kuhakikisha Kila Mwananchi Anapata Huduma Bora Na Salama

 

Ameyasema Hayo Katika Hafla Fupi Ya Ufunguzi Wa Mradi Wa Mji Safi Na Salama Skimu Ya Dole Amesema Mradi Huu Unaozinduliwa Ni Moja Ya Mafanikio Katika Uimarishaji Wa Maji Safi Na Salama.

NI FARAJA KUBWA KUONA WAZANZIBARI WANAJIVUNIA MATUNDA YA MAPINDUZI NA HUDUMA BORA

Waziri Mkuu Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Ameipongeza Wizara Ya Afya Kwa Kuweza Kutekeleza Sera Ya Afya Na  Kusimamia Vyema Miradi Ya Wizara Ya Afya.

 

Akifungua Hospitali Ya Wilaya Kaskazini B Pangatupu Ikiwa Ni Shamrashamra Za Miaka 60 Ya Mapinduzi  Ya Zanzibar Amesema Ni Faraja Kubwa Kuona Wazanzibari Wanajivunia Matunda Ya Mapinduzi Na Huduma Bora Za Kibingwa Zinapatikana 

NCHI INAENDELEA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA IKIWA NI MIONGONI MWA DHAMIRA YA MAPINDUZI YA MWAKA 1964.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Nchi inaendelea kuimarisha huduma za afya ikiwa ni miongoni mwa dhamira ya Mapinduzi ya mwaka 1964.

Akizungumza wakati alipozinduwa Hospitali ya Mkoa wa Mjini Magharibi huko Lumumbakatika shamra shamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Samia amesema kwa vile Hospitali hiyo itatoa huduma bora na za kisasa ni vyema watendaji na wahusika wa hospitali kuhakikisha huduma zinazotolewa kwa Wananchi zinaimarika kuwa bora zaidi.

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KITAENDELEA KUWAMINI VIJANA KAMA NYENZO MUHIMU YA UTAYARI KATIKA MAENDELEO NA MIPANGO YA SERIKALI.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi  Taifa Dkt. Samia Suluhu Hassan  amesema Chama hicho kitaendelea kuwamini Vijana kama nyenzo muhimu ya utayari katika Maendeleo na Mipango ya Serikali.

Mwenyekiti huyo wa CCM ambae ni Rais wa Jamuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza baada ya kupokea matmbezi ya umoja wa Vijana wa CCM ikiwa ni kilele cha matembezi hayo huko maisra, amesema kwa msingi huo Vijana wanapaswa kujengewa uwezo pamoja na kuendeleza vipaji vyao huku akiwataka kujitambua.

VIONGOZI WA JUMUIYA YA UMOJA WA VIJANA UVCCM KATIKA HAFLA YA CHAKULA CHA USIKU

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi amejumuika pamoja na Viongozi  wa jumuiya ya umoja wa Vijana UVCCM katika hafla ya Chakula cha usiku

Akizungumza na Vijana  katika hafla hiyo Rais Dk.Mwinyi amesema

Serikali na Chama cha Mapinduzi wamefarajika  kwa kuungwa mkono katika sherehe  za miaka 60 ya Mapinduzi matukufu ya

Zanzibar.

KAMPUNI YA UJENZI YA SERIKALI YA CHINA [CCECC] KUTEKELEZA MAAGIZO YA SMZ

Kampuni ya ujenzi ya Serikali ya China CCECC imesema itaendelea kutekeleza maagizo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuimarisha Miundombinu ya usafiri ili kuondoa tatizo la Miundombinu liliopo Nchini. 

Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya CCECC Tanzania na Afrika Mashariki Zhang junle akizungumza na waandishi wa habari huko Serena Hotel amesema Serikali ya China inaipongeza SMZ kwa kuendelea kuiyamini katika ujenzi wa Miradi ya Barabara inayoendelea na kuahidi kumaliza kwa wakati 

WATU WATATU WA FAMILIA MOJA WAMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUZAMA MAJI

Watu Watatu wa Familia moja Wamefariki Dunia baada ya kuzama Maji  kufuatia Mvua iliyonyesha majira ya saa saba usiku na kusababisha Maafa.

Akithibitisha kuokolewa kwa Miili ya Watu hao Wawili Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Morogoro  Shabani Marugujo amesema kuwa bado wanaendelea na jitihada za kuutafuta Mwili wa Mtu mmoja ambaye mpaka sasa haujapatikana.

Amesema kuwa Nje ya Miili hiyo Mtu mmoja  wa familia hiyo amefanikiwa kujiokoa na kukimbizwa Hospitali kwaajili ya Matibabu.

MAZINGIRA WEZESHI KWA WAWEKEZAJI

Serikali imesema itaendelea kuweka Mazingira wezeshi ya uwekezaji wa Kitanzania ili waweze kunufaika na fursa zinazotolewa na Kituo cha uwekezaji Tanzania TIC ikiwemo punguzo la asilimia 75 kwenye Vifaa vinavyotumika katika  uwekezaji

Kauli hiyo imesemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha uwekezaji Tanzania [TIC] Gilead Teri alipotembelea wawekezaji Jijini mwanza ndipo akaona ipo haja ya kuwawekea mazingira wezeshi ili wafanye shughuli zao kwa ufanisi

WANANCHI WILAYA YA KUSINI KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA

Mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Kamishna Ayoub Bakari Hamad amewataka Wananchi wa Wilaya ya Kusini kuendelea kujitokeza kujiandikisha katika Daftari la kudumu la Wapiga kura linaloendelea katika wilaya hiyo

Akizungumza baada ya kukagua Vituo vya uandikishaji Wapiga Kura wapya katika Wilaya ya Kusini amesema hatua hiyo itawawezesha kutumia haki yao ya Democrasia ikiwemo kupiga kura katika uchaguzi mkuu. 

Afisa uandikishaji Wilaya ya Kusini Samson Ezekel Kibona amesema kazi hiyo inaendelea vizuri ambapo Jumla ya Vituo 21 vimetumika kuandikisha Wapiga kura wapya.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.