Habari

UCHUMI WA ZANZIBAR UMEIMARIKA KUTOKA TRILIONI 3 NUKTA 116 MWAKA 2020 NA KUFIKIA TRILIONI 3.499 MWAKA 2022.

Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi Katika Hutuba Yake Kwa Umma Usiku Wa Kuamkia Kilele Cha Mapinduzi Amesema Ongezeko Hilo Limechangiwa Na Masuala Mengi Ikiwemo Uwekezaji.

Hata Hivyo Ukusanyaji Mapato Nao Umeongezeka Kufikia Trilioni 1.4 Mwaka 2022/2023 Kutoka Bilioni 790.48 Mwaka 2020/2021.

 

WAKALA WA BARABARA NCHINI ( TANROADS) MKOA WA MWANZA UMEWATAKA WAKANDARASI WANAOENDELEA NA MATENGENEZO YA BARABARA ZILIZOKUWA HAZIJAJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI KUHARAKISHA ILI KUMALIZIKA KWA WAKATI.

Kampuni Za Wakandarasi Wazawa Zinazoendelea Na Matengenezo Ya Barabara Za Kiwango Cha Changarawe Katika Halmashauri Za Buchosa, Sengerema Na Ukerwe Ni Sita, Ambazo Ni Lean Engineers Ltd Ya Dar Es Salaam, Samota Ya Nzega, Jonta Investment Ltd Ya Shinyanga, Am & Partner Ltd Ya Dar Es Salaam, Kasco Ltd Ya Mwanza Na Cym Contractors Ltd Ya Singida.

Meneja Wa Tanroads Mkoa Wa Mwanza Mhandisi Paschal Ambrose Amesema Matengenezo Ya Barabara Hizo Zenye Urefu Wa Kilometa Zaidi Ya Mia Tatu Yanatarajia Kukamilika Kabla Ya Juni 30 Mwaka Huu.

MKUU WA WILAYA YA KISHAPU JOSEPH MKUDE AMEFANYA MSAKO WA KUSHITUKIZA KATIKA MNADA WA MHUNZE NA KUKAMATA WANAFUNZI 45 AMBAO WALIKUWA WAKIZURURA NA KUAGIZA KUTAFUTWA WANAFUNZI AMBAO HAWAJARIPOTI SKULI ILI WAANZE MASOMO

Hatua Hiyo Ya Mkuu Wa Wilaya Imetokana Na Kufanya Ukaguzi Katika Skuli Ya Sekondari Isoso Hivi Karibuni Na Kukutana Na Wanafunzi Sita Ambao Wameripoti Kati Ya 138 Waliopangiwa Katika Skuli Hiyo.

Akitoa Taarifa  Mkuu Wa Skuli Ya Sekondari Isoso Anusiata Audax Amesema Mwitikio Wa Wazazi Kupeleka Watoto  Waliochaguliwa Kujiunga Kidato Cha Kwanza Ni Mdogo.

WAFANYABISHARA 18 WA WILAYA YA HANANG MKOA WA MANYARA WALIOKUWA WATEJA WA BENKI YA NMB AMBAO BIASHARA ZAO ZIMEATHIRIWA NA MAPOROMOKO YA UDONGO MWAKA JANA WAMELIPWA FIDIA YA SHILINGI MILIONI 269 NUKTA 7 KAMA FIDIA YA BIASHARA ZAO.

Akizungumza Katika Hafla Ya Utoaji Hundi Ya Fidia Hiyo Kutoka Kampuni Ya Bima Ya Reliance Tanzania Meneja Wa NMB Kanda Ya Kaskazini Ametoa Wito Kwa Wafanyabishara Wengine Nchini Kuona Umuhimu Wa Kukatia Bima Biashara Zao. 

Mkuu Wa Wilaya Ya Hanang Janet Mayanja Amewapongeza Wateja Wa Benki Ya NMB Kwa Kukumbuka Kukata Bima Na Kuwataka Wengine Kuiga Mfano Huo, Huku Kamishna Mkuu Wa Mamlaka Ya Bima Tanzania Dkt Baghayo Saqware Ametoa Wito Kwa Watanzania Kuona Umuhimu Wa Bima Katika Kila Biashara Wanazozifanya. 

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALI ASILI NA UTALII IMESEMA IMERIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA NYUMBA MPYA KATIKA KIJIJI CHA MSOMERA WILAYA YA HANDENI MKOA WA TANGA

Akizungumza Baada Ya Kamati Hiyo Kutembelea Na Kukagua Ujenzi Wa Miundombinu Ikiwemo Nyumba Kwenye Kijiji Hicho Cha Msomera, Mwenyekiti Wa Kamati Hiyo Timotheo Mzava Amesema Ujenzi Umezingatia Viwango.

Kamanda Wa Oparesheni Ya Ujenzi Wa Nyumba Hizo Za  Msomera Kanali Sadick Mihayo Amesema Watahakikisha Wanamaliza Ujenzi Huo Kwa Wakati,Ili Wageni Wanaoletwa Waweze Kupata Makazi Haraka.

Mkuu Wa Wilaya Ya Handeni Albert Msando Ameeleza Kuwa Licha Ya Ujenzi Wa Nyumba,Ipo Baadhi Ya Miundombinu Ya Huduma Za Kijamii Nayo Inatengenezwa Kama Anavyoeleza..

MKURUGENZI MTENDAJI WIZARA YA AFYA KHAMIS HAMAD SULEIMAN AMEWAHIMIZA WANANCHI KUJITOKEZA KUCHANGIA DAMU ILI KUISAIDIA JAMII.

Akitoa Shukurani Kwa Taasisi Ya Majlis Al-Maarif Mara Baada Ya Kupokea Vifaaa Vya Kushajihisha Uchangiaji Damu, Mkurugenzi Huyo Amesema Mahitaji Ya Damu Yameongezeka Kulingana Na Ongezeko La Majengo Ya Hospitali Hivyo Kuna Umuhimu Wa Kuchangia Damu.

Mwenyekiti Wa Taasisi Ya Majlis Almaarif Tahir Khatib Tahir Amezitaka Taasisi Za Dini, Chama Na Serikali Kujitokeza Kuchangia Damu Ili Kuhakikisha Wanaohitaji Waweze Kupata Huduma Hiyo Kwa Uhakika.

SERIKALI IMESEMA INA NIA YA KULIBADILISHA ENEO LA DIMANI KUWA LA KIBIASHARA LA KIMATAIFA.

Akifungua Maonesho Ya 10 Ya Biashara Ya Kimataifa, Rais Wa Zanzibar Na Mwenyekiti Wa Baraza La Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi Ikiwa Ni Mwendelezo Wa Shamrashamra Za Miaka 60 Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Dk Mwinyi Amesema Serikali Imekusudia Kujenga Majengo Mbali Mbali Ya Kisasa Ya Biashara Na Kwa Sasa Wameanza Na Eneo La Nyamanzi Wilaya Ya Magaharbi B, Ambapo Tayari Kashakabidhiwa Mfano Wa Ramani Ya Mji Mpya Wa Biashara Na Uwekezaji Wa Eneo Hilo Waziri Wa Biashara Na Maendeleo Ya Viwanda Wa Zanzibar.

DKT. HUSSEIN ALI MWINYI AMEWATUNUKU NISHANI VIONGOZI MBALI MBALI WALIOTUMIKIA SERIKALI KWA MIAKA KADHAA.

Sherehe Za Kuwatunuku Nishani Viongozi Hao Zimefanyika Katika Viwanja Vya Ikulu Mjini Zanzibar Katika Maadhimisho Ya Miaka 60 Ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt Mwinyi Amemtunuku Nishani Ya Mapinduzi Ya Kiongozi Mwenye Sifa Ya Kipekee Rais Wa Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzani Dkt Samia Suluhu Hassan. 

Nishani Nyengine Ni Viongozi Na Wananchi Wenye Sifa Maalum Ambapo Dkt Muhamed Gharib Bilal, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha, Balozi Seif Ali Iddi Na Marehemu Seif Sharif Hamad Wamekabidhiwa Nishani Hizo.

 

MWINYI AMETOA MSAMAHA NA KUWAACHIA HURU WANAFUNZI ISHIRINI NA SITA WALIOKUWA WAKITUMIKIA CHUO CHA MAFUNZO KWA UNGUJA NA PEMBA.

Dk Mwinyi Ametoa Msamaha Huo Chini Ya Kifungu 59 Cha Katiba Ya Zanzibar Ya Mwaka 1984 Ikiwa Ni Kusherehekea Miaka 60 Ya Mapinduzi Ya Zanzibar.

Msamaha Huo Umewahusu Wanafunzi Kumi Na Tano Kutoka Unguja Na Kumi Kutoka Pemba.

Msamaha Kama Huo Hutolewa Kila Mwaka Kwa Baadhi Ya Wanafunzi Wa Chuo Cha Mafunzo.

 

DKT JAKAYA KIKWETE AMESEMA MASUALA YA UCHUMI YATAIBUA MIRADI YA UWEKEZAJI.

Rais Mstaafu Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania   Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Amesema Kuwepo Sera Na Mipango Bora Katika Usimamizi Wa Masuala Ya Uchumi, Kumesababisha Kuibuka Miradi Zaidi Ya Uwekezaji Yenye  Tija.

 

Akizungumza Katika Hafla Ya Uwekaji Jiwe La Msingi Hoteli Ya Jazz Aurora Huko Michamvi, Amesema Hatua Hiyo Pia Imesaidia Kuipa Nafasi Ya Kipekee Sekta  Ya Biashara Na Uwekezaji Kwa Kuleta Matokeo Mazuri.

 

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.