DKT JAKAYA KIKWETE AMESEMA MASUALA YA UCHUMI YATAIBUA MIRADI YA UWEKEZAJI.

Dkt Jakaya  Kikwete

Rais Mstaafu Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania   Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Amesema Kuwepo Sera Na Mipango Bora Katika Usimamizi Wa Masuala Ya Uchumi, Kumesababisha Kuibuka Miradi Zaidi Ya Uwekezaji Yenye  Tija.

 

Akizungumza Katika Hafla Ya Uwekaji Jiwe La Msingi Hoteli Ya Jazz Aurora Huko Michamvi, Amesema Hatua Hiyo Pia Imesaidia Kuipa Nafasi Ya Kipekee Sekta  Ya Biashara Na Uwekezaji Kwa Kuleta Matokeo Mazuri.

 

Amesema Duniani Hakuna Uchumi Unaokuwa Bila Ya Uwekezaji Ambapo Wawekezaji Huwekeza Kupitia Mitaji Mikubwa Na Kuweza Kulipa Kodi Vizuri Serikalini,  Na Kushauri Serikali Kusimamia Wananchi Kuzalisha Bidhaa  Zitakazouzika Katika Za Kitalii.

 

Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Rais Kazi, Uchumi Na Uwekezaji, Mh Mudrik Ramadhan Soraga, Amesema Ili Kuwa Na Uwekezaji Suala La Amani Na Utulivu Lina Umuhimu Mkubwa, Hivyo Amewtaka Wananchi Kuendelea Kutunza Amani  Ili Kutoa Fursa Zaidi Za Miradi.

 

Nae Mkurugenzi Wa Mradi Huo Wa Jazz Aurora, Bw. Diego Torrado ,  Amesema Wametoa Mafunzo Maalum Kwa Vijana Wa Eneo Hilo Wapatao Mia Tano, Ambapo Tayari Wamewapatia Ajira Mbali Mbali Katika Hoteli Hiyo.

 

Zaidi Ya Dola Milioni Hamsini Zitatumika Katika Ujenzi Wa Mradi Huo Hadi Kukamilika Kwake.

  

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.