Habari

KUWEPO KWA KAMBI MAALUM ZA KUWALEA VIJANA KATIKA MAADILI MEMA KUTASAIDIA KUIOKOA JAMII DHIDI YA VITENDO VIOVU NA KUJENGA JAMII ILIYO BORA.

Akizungumza Katika Hafla Ya Uzinduzi Wa Kambi Ya Maadili Kupitia Jumuiya Ya Malezi Ya Kiislam Elimu Na Maadili Zanzibar  Mlezi Wa Jumuiya Hiyo Jaji Mshibe Ali Bakari Amesema Athari Zinazoikumba Jamii Zinatokana Na Kukosa Elimu Pamoja Na Maadili Mema.

 

Akisoma Risala Kwa Niaba Ya Washiriki Wa Kambi Hiyo Khamis Ali Khamis Amesema Kambi Hiyo Imeandaliwa Ili Kuwajenga Kitabia Na Kutambua Lengo La Kuumbwa Kwao Pamoja Na Kujilinda Na Athari Zinazoweza Kuwakumba Na Kuhatarisha Maisha Yao.

 

KUNA UMUHIMU WA KUWEKA MIKAKATI MADHUBUTI JUU YA KUSHUGHULIKIA MATATIZO YA AFYA YA AKILI ILI KUPUNGUZA MADHARA YATOKANAYO NA MAGONJWA HAYO.

Mh. Mattar Ameyasema Hayo Wakati Alipokuwa Akifungua Mafunzo   Juu Ya Namna Ya Kutoa Taaluma Ya Afya Ya Akili, Yaliyowashirikisha  Madakta Pamoja Na Watendaji Wa Kada Mbali Mbali Za Afya Huko Katika Ukumbi Wa Maabara Ya Afya Ya Jamii Wawi Kisiwani Pemba.

Amesema, Hivi Sasa Kuna Matatizo Mengi Yanayosababishwa  Na Magonjwa Ya Afya Ya Akili,  Hivyo Ni Vyema Kuhakikisha Suala La Afya  Ya Akili Linapewa Umuhimu Mkubwa Huku Jamii Ikiacha Unyanyapaa Kwa Watu Wenye Matatizo Hayo.

ASASI ZA KIRAIA ZIMESHAURIWA KUOMBA MIRADI KWENYE SHIRIKA LA DANMISSION

Asasi Za Kiraia Zanzibar Zimetakiwa Kutumia Fursa Zinazotolewa Na Mashirikaka Ya Nje Katika Kutekeleza Miradi Yao Ya Kusaidia Jamii.

 

Mrajis Wa Asasi Hizo Ahmed Khalid Abdullah Ameeleza Hayo Katika Mkutano Wa Kulitambulisha Shirika La Danmission, Lenye Lengo La Kutoa Ufadhili Wa Miradi Kwa Asasi Za Zanzibar, Amesema Ni Vyema  Kwa Asasi Zikatumia Fursa Za Ufadhili Wa Miradi Zinazotolewa Na Shirika Hilo.

 

KUIMARIKA KWA BIMA KUTALETA USHINDANI SOKO LA BIASHARA

Kuimarika kwa huduma bora za Bima Zanzibar kutazidi kuleta maendeleo kwa Wananchi wake.

 Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya wa Shirika la Bima Zanzibar ZIC Waziri Ofisi ya Rais fedha na mipango Dk Sada Mkuya Salum amesema hatua hiyo itazidi kuimarisha ushindani katika Soko la kibiashara amesema Mapinduzi ya Kiuchumi Zanzibar yanalengo la kuleta maendeleo kwa Wananchi wake huku akizidi kutoa wito kwa Jamii kukata bima kwa maslahi ya mali zao.

ZRA KUJITATHMINI KWA KUONGEZA MAKUSANYO YA KODI.

Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi  Zena  Ahmed Said amesema  hayo katika Mkutano wa  kutathmini utendaji na kupanga mikakati ya ukusanya Kodi kwa nusu ya pili kwa Mwaka 2023/2024 huko Hotel ya Madinatul Bahar Mbweni Mjini Unguja.

Amesema usimamizi mzuri kwa Watendaji kunasaidia kuleta ufanisi katika kazi na kuimarika kwa mifumo ya ukusanyaji wa Mapato kunaharakisha maendeleo ya Taifa.

DKT HUSSEIN ALI MWINYI AMEPONGEZWA NA VIONGOZI MBALIMBALI WALIOFIKA IKULU ZANZIBAR.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi amepongezwa na Viongozi mbalimbali waliofika Ikulu Zanzibar kwa sherehe zilizofanywa za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Majeshi ya ulinzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania CDF Jenerali Jacob John Mkunda alipokutana na kufanya mazunguzu na Dkt Mwinyi Ikulu.

ZANZIBAR SCHOOL OF HEALTH NI MATUNDA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA MWAKA 1964

Rais Mstaafu  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt  Jakaya Mrisho Kikwete amesema Chuo  Cha Afya  Cha Zanzibar School  Of Health ni moja  ya Matunda ya  Mapinduzi ya Zanzibar ya  kuhakikisha Wananchi wake wanapata huduma za afya  zilizo bora.

Akizungumza  katika Mahafali ya 11 ya Wanafunzi wa  Chuo hicho  amesema katika Sekta ya afya bado kuna pengo  kubwa la Wataalamu hivyo Chuo hicho kinawajibu wa  kuzalisha Wataalamu ambao watatoa huduma  kwa  Jamii.

SMT NA SMZ KUIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA TAASISI ZA UMMA

Kufanyika kwa Mkutano wa Wakuu wa Taasisi za SMT na SMZ kutasaidia kuimarisha ushirikiano kati ya Taasisi za Umma Visiwani Zanzibar na tanzania Bara..

Akifungua Mkutano wa Wakuu wa Taasisi za SMT na SMZ katika kusherehekea Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema Serikali zote Mbili zimeamuwa kuanzisha Mkutano huo ili Wakuu wa Taasisi za Umma waweze kubadilishana uzoefu na kujadili namna bora za kuimarisha Taasisi hizo ili kuliletea Taifa Maendeleo. 

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA IMEWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI KIPINDI HIKI CHA MVUA

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Ofisi ya Zanzibar Masoud Makame Faki ametoa tahadhari hiyo alipozungumza na ZBC katika Viwanja vya maonesho ya biashara Nyamanzi Wilaya ya Magharib B.

Amesema Mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa zinaambatana na Upepo mkali pamoja na Radi hivyo ni vyema kuchukua tahadhari kwa Wavuvi na Familia zinazoishi maeneo hatarishi.

ZAIDI YA WATU ELFU 19 WANATARAJIWA KUANDIKISHWA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KWA WILAYA YA MJINI.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji George Joseph amesema hayo katika siku ya kwanza ya uwandishaji wa Wapiga Kura wapya  Wilaya ya Mjini 

Amesema idadi hiyo itaongeza ya Wapiga kura kwa Mkoa Mkoa wa Mjini Magharibi.   

Mjumbe wa Tume ya Taifa ya uchaguzi NEC Mwanaisha Kwalikwa amesema maandalizi ya uwandikishaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura yanaenda vyema na kuwaomba Wananchi  kujitokeza   kujiandikisha  ili kutimiza haki yao ya Democrasia

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.