Habari

CHAMA KITAHAKIKISHA KINAWAPIMA VIONGOZI WAKIWEMO WABUNGE NA WAWAKILISHI KATIKA CHAGUZI ZA CHAMA ZITAKAPOKARIBIA.

Dk. Samia Ameyasema Hayo  Katika Ziara Yake Ya Kichama  Katika Mkoa Wa Kaskazini Unguja, Wakati Akifungua Tawi La CCM Chaani Masingini Na Kufungua Kituo Cha Ushoni Cha Wanawake Mahonda, Amesema Viongozi  Ambao Wapo Nyuma Kikazi Hawana Budi Kutekeleza Majukumu Yao Kwa Kipindi Kilichobaki. 

 

SERIKALI ITAENDELEA KUWAPATIA HUDUMA BORA ZA MATIBABU WANANCHI KWA KUWAJENGEA MAJENGO NA VIFA VYA KISASA.

Akizungumza Wakati Alipofungua Jengo La Huduma Za Tiba Za Dharura Na Maabara Huko Makunduchi Dkt Mwinyi Amesema, Katika Mwaka Wa Fedha 2023/2024 Serikali Imekusudia Kujenga Majengo Mapya Na Vifaa Tiba Vya Kisasa Ili Kuhakikisha Zinapatikana Kwa Wakati.

 

Amesema Kujengwa Kwa Jengo Hilo Itasaidia Kupatikana Kwa Wakati Huduma Za Afya Na Kupunguza Vifo. 

 

JUMLA YA WATU 15 WAMEOKOLEWA NA MMOJA KUJERUHIWA KUFUATIA KUANGUKA KWA JENGO LILILOKUWA LIKIFANYIWA MATENGENEZO KATIKA ENEO LA FORODHANI

Katika Ajali Hiyo Iliyotokea Majira Ya Mchana, Jengo Hilo Lililoporomoka Ambalo Lilikuwa Benki Ya PBZ, Lipo Katika Matengenezo Na Wakati Ajali Inatokea Watu 16 Walikuwemo Ndani Ya Nyumba Hiyo, Majeruhi Ambae Alifunikwa  Akitambuliwa Kwa Jina La Mayani Mussa Bakari  Anasadikiwa Kuwa Na Miaka 35 Aliokolewa Kwa Msaada Wa Kikosi Cha Zimamoto Na Uokozi.

 

TAASISI ZA UMMA ZIMETAKIWA KUHAKIKISHA ZINASIMAMIA NA KUTEKELEZA MATAKWA YA SHERIA KATIKA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA

Kauli Hiyo Imetolewa Na Kamati Ya Kuchunguza Na Kudhibiti Hesabu Za Serikali PAC, Wakati Walipokua Wakipokea Majibu Ya Hoja Zilizotolewa Na Mdhibiti Na Mkaguzi Mkuu Wa Hesabu Za Serikali, Zinazohusu Dosari Zilizojitokeza Katika Mradi Wa Ujenzi Wa Vyumba Vya Kusomea Katika Chuo Cha Kiislamu Micheweni Pemba.

 

TAASISI ZA HAKI JINAI ZIMETAKIWA KUSHIRIKIANA NA KUSHUGHULIKIA KESI KATIKA KUTOA HAKI KWA MUJIBU WA SHARIA.

Wito Huo Umetolewa Na Mwenyekiti Wa Kamati Ya Viongozi Wakuu Wa Kitaifa Ya Baraza La Wawakilishi Mhe. Machano Othman  Said, Huko Ofisi Ya Mkurugenzi Wa Mashtaka Chake Chake Katika Kikao Cha Uwasilishwaji Wa Tarifa Za Utekelezaji Wa Ofisi Ya Rais Katiba Sheria Na Utumishi Wa Umma Katika Kipindi Cha Robo Mwaka.

 

Amesema Wizara Hiyo Ndio Yenye Jukumu Kubwa La Kuhakikisha Inasimamia  Haki Za Wananchi Kwa Kupata Haki Zao Na Kuilinda Serekali Katika Kuwahudumia Wananchi Hivyo Ni Vyema  Kutoa Haki Kwa Kufuata Misingi Ya Sheria.

 

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR IPO KATIKA MPANGO WA KUFANYA UTAFITI KUPITIA SEKTA YA UTALII ILI UTALII UWEZE KUWA ENDELEVU BILA YA KUIATHIRI JAMII, URITHI WA KALE, TAMADUNI ZA KIZANZIBARI NA MAZINGIRA.

Akizungumza Katika Kikao Kazi Cha Wataalamu Na Wadau Wa Utalii Katibu Mkuu Wizara Ya Utalii Na Mambo Ya Kale Fatma Mbarouk Khamis, Amesema Lengo La Utafiti Huo Wa ZTCC Ni Kutathmini Uwezo Wa Zanzibar Wa Kuhimili Watalii Wanaoingia Nchini Pasipo Kuleta Madhara Yoyote Kwa Nchi Na Wananchi.

 

WANANCHI WANAONG’OA VIBANGO VYA UTAMBULISHO WA MAJINA YA MITAA NA NAMBA ZA NYUMBA KUWACHA TABIA HIYO.

Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makaazi ya Mwaka 2022 Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameyasema hayo katika Kikao cha kumi 10  cha Kamati Kuu ya Kitaifa ya Sensa ya Watu na Makaazi ya Mwaka 2022 Mhe Majaaliwa amesema Tamisemi kwa pande zote mbili zina wajibu wa  kufuatilia  na kuhakikisha Vibao vya Anuani za Majina ya Mitaa havibanduliwi na vinabaki katika uhalisia ili kumrahisishia Mwananchi kufika sehemu husika bila ya usumbufu wa aina yoyote.

TUME YA UCHAGUZI NEC KUFANYAKAZI KWA USHIRIKIANO

Mwenyekiti Tume ya Taifa ya uchaguzi Tanzania Mh Jaji Jacob Mwambegele amesema Tume ya uchaguzi inahitaji kufanyakazi kwa ushirikiano ili kuifahamisha Jamii majukumu yanayofanywa na Tume hiyo.

Mwenyekiti huyo wa Tume ya Uchaguzi, akiwa katika maonesho ya kumi ya Biashara yanayofanyika Nyamanzi Wilaya ya Magharibi B, amesema lengo la kuwepo kwenye maonesho lifahamke na Wananchi ili kutoa nafasi ya kutembelea na kupata huduma.

ZAIDI YA WAGENI 2000 KUTOKA NCHI MBALI MBALI DUNIANI WAMEWASILI NCHINI KWA LENGO LA KUTALII KUPITIA MELI KUBWA YA NORWEGIAN DAWN IKITOKEA KENYA NA KUELEKEA DAR ES SALAAM.

Akizungumza Na Vyombo Vya Habari Katika Meli Hiyo, Waziri Wa Utalii Na Mambo Ya Kale Mhe. Simai Mohamed Said, Amesema Malengo Ya Serikali Ya Kuitangaza Zanzibar Kiutalii Yanafanikiwa Kutokana Na Kuwasili Kwa Meli Za Kimataifa Hatua Inayochangia Kukuza Pato La Taifa. 

 

Kepten Wa Meli Hiyo Asen Gyruv, Amesema Wamevutiwa Kuja Kutembea Zanzibar Kutokana Na Uzuri Wa Mandhari Yake Ya Asili Na Ukarimu Wa Watu Wake, Na Kuahidi Kuifanya Zanzibar Kuwa Miongoni Mwa Vituo Vya Kushusha Abiria.

 

HATUA ZILIZOFIKIWA ZA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI INAYOJENGWA KATIKA MAENEO MBALI MBALI NCHINI INARIDHISHA.

Hayo Yameelezwa Na Wajumbe Wa Kamati Ya Mawasilianio, Ardhi Na Nishati Ya Baraza La Wawakilishi, Chini Ya Makamo Mwenyekiti Wake Mhe Azza Januar Joseph, Wameyaeleza Hayo Wakati Walipotembea Miradi Mbali Mbali Ya Maji Na Kupokea Taarifa Ya Utekelezaji Wa Bajeti Ya Mamlaka Ya Maji Zanzibar (ZAWA) Kwa Kipindi Cha Julai Hadi Disemba 2023 .

 

Wameilekeza Wizara Ya Maji Kuhakikisha Inaendelea Kuisimamia Kwa Karibu Ujenzi Wa Miradi Hiyo Nchini Kote Ili Miradi Mingi Itekelezwe Kwa Ubora Na Kukamilika Kwa Wakati Na Hatimae  Dhamira Ya Serikali Itimie Kikamilifu.

Subscribe to Habari
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.