ZANZIBAR SCHOOL OF HEALTH NI MATUNDA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR YA MWAKA 1964

RAIS MSTAAFU WA TANZANIA MH JAKAYA MRISHO KIKWETE

Rais Mstaafu  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt  Jakaya Mrisho Kikwete amesema Chuo  Cha Afya  Cha Zanzibar School  Of Health ni moja  ya Matunda ya  Mapinduzi ya Zanzibar ya  kuhakikisha Wananchi wake wanapata huduma za afya  zilizo bora.

Akizungumza  katika Mahafali ya 11 ya Wanafunzi wa  Chuo hicho  amesema katika Sekta ya afya bado kuna pengo  kubwa la Wataalamu hivyo Chuo hicho kinawajibu wa  kuzalisha Wataalamu ambao watatoa huduma  kwa  Jamii.

Mkurugenzi Mtendaji wa Zanzibar School of Health  Aziza Hamed amesema  Zanzibar School of Health  inadhamiria  kuchangia  kuwandaa Vijana  ili kutoa huduma za  Afya  na kujiajiri.

Naibu Waziri wa  Elimu Zanzibar  Mhe, Ali Abdul-ghulam Hussein amesema Serikali   itaendelea kutoa ushirikiano kwa Taasisi Binafsi katika maendeleo.

Jumla  ya Wahitimu Miatano ishirini na  sita wamehitimu na  kutunukiwa  Vyeti 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.