MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA IMEWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI KIPINDI HIKI CHA MVUA

MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Ofisi ya Zanzibar Masoud Makame Faki ametoa tahadhari hiyo alipozungumza na ZBC katika Viwanja vya maonesho ya biashara Nyamanzi Wilaya ya Magharib B.

Amesema Mvua zinazoendelea kunyesha hivi sasa zinaambatana na Upepo mkali pamoja na Radi hivyo ni vyema kuchukua tahadhari kwa Wavuvi na Familia zinazoishi maeneo hatarishi.

Kaimu Meneja Masomo na Uhusiano wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Monica motony amewataka Wananchi kufika katika Banda la Mamlaka hiyo ili kupata Taaluma mbalimbali kuhusu hali ya Hewa na tahadhari zake.

Maenesho ya Kimataifa ya Kibiashara yanaendelea katika Viwanja vipya vya maonesho Nyamanzi na yanatarajiwa kufungwa tarehe 19 ya Mwezi huu.

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.