Mh. Mattar Ameyasema Hayo Wakati Alipokuwa Akifungua Mafunzo Juu Ya Namna Ya Kutoa Taaluma Ya Afya Ya Akili, Yaliyowashirikisha Madakta Pamoja Na Watendaji Wa Kada Mbali Mbali Za Afya Huko Katika Ukumbi Wa Maabara Ya Afya Ya Jamii Wawi Kisiwani Pemba.
Amesema, Hivi Sasa Kuna Matatizo Mengi Yanayosababishwa Na Magonjwa Ya Afya Ya Akili, Hivyo Ni Vyema Kuhakikisha Suala La Afya Ya Akili Linapewa Umuhimu Mkubwa Huku Jamii Ikiacha Unyanyapaa Kwa Watu Wenye Matatizo Hayo.
Kwa Upande Wake Afisa Mdhamini Wizara Ya Afya Pemba Khamis Bilal Ali, Amelishukuru Shirika La Kuboresha Afya Zanzibar Kwa Kuiyunga Mkono Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Katika Kuwahudumia Wananchi Wake Hasa Katika Muasula Ya Afya.
Akizungumzia Kuhusu Lengo La Mafunzo Hayo Mratib Wa Shirika Hilo Pemba Abdalla Omar Abdalla Amesema, Hivi Sasa Kuna Watu Wengi Ambao Wanasumbuliwa Na Msongo Wa Mawazo Ambayo Husababisha Watu Kuugua Na Hata Kujinyonga Hivyo Hips Inatoa Mafunzo Hayo Ili Kushirikiana Na Wizara Ya Afya Kuondoa Kabisa Tatizo Hilo.
Mafunzo Hayo Ya Siku Nane Yanaendeshwa Kwa Mashirikiano Ya Pamoja Kati Ya Shirika La Kuboresha Afya Hips Na Wizara Ya Afya Zanzibar.