Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, ameshiriki katika Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (Joint Permanent Commission - JPC) kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Uganda uliofanyika kwa lengo la kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika sekta mbalimbali za maendeleo.
Katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, wajumbe wamejadili masuala mbalimbali ikiwemo mashirikiano ya kidiplomasia na kisiasa, masuala ya ulinzi na usalama pamoja na uhamiaji.