WATENDAJI KITUO CHA UOKOZI MWANZA WATAKIWA KUTOA HUDUMA ZA DHARURA KWA SAA 24
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa maagizo kwa watendaji wa Kituo cha Kuratibu. Utafutaji na Uokozi cha Kikanda β Mwanza, chenye thamani ya takribani shilingi bilioni 19.8, kuhakikisha kituo hicho kinaendeshwa kwa saa 24 na kwa ufanisi wa hali ya juu.
Amesema hayo leo Januari 23, 2026 baada ya kutembelea kituo cha Kuratibu Utafutaji na Uokozi, jijini Mwanza. Huku akisisitiza kuwa huduma za uokozi ni kazi ya kuokoa maisha, hivyo hakuna uvumilivu kwa uzembe, kuchelewesha utoaji wa huduma za msaada pindi inapohitajika.

