SERIKALI YAAHIDI KUTOA KIWANJA UJENZI OFISI ZA MAHUJAJI SAUDI ARABIA

Dkt.Mwinyi Mahujaji

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi ameahidi Serikali kutoa kiwanja kwa ajili ofisi za kudumu za Mahujaj wanaojiandaa kwenda kushiriki ibada ya Hijja nchini Saudi Arabia.

     Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika hafla fupi ya kuwaaga Mahujaj wanaokwenda ibada ya Hijja nchini Saudi Arabia iliyofanyika Msikiti wa Jaamiu Zinjibar Mazizini, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 23 Mei 2024.

    Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali itaendelea kukaa na wadau ili kuongeza kipato cha kupeleka watu Hijja pia kuweka utaratibu mzuri wa michango kidogo kidogo mapema.

     Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali itazungumza na Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia ili kusaidia kuweka ofisi ya kudumu kupokea Mahujaj wanaokwenda nchini humo.

   Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewaomba Mahujaj kuiombea dua nchi na viongozi wake ili kuendelea kupata mafanikio yaliyotarajiwa na kudumisha amani.

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.