UJENZI WA KITUO CHA UMEME URAMBO ASILIMIA 92 ZAFIKIWA

Tanesco

  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhe. Gissima Nyamo-Hanga ametembelea na kukagua maendeleo ya utekelezaji wa ujenzi wa kituoa cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme cha Uhuru - Urambo ( Kilovolti 132) mkoani Tabora ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe.Dkt Doto Biteko aliyoyatoa Machi 27, 2024  alipotembelea mradi huo na kusisitiza usimamizi wa karibu ili kuhakikisha  mradi unakamilika kwa wakati uliopangwa

    Mhandisi Gissima amesema kuwa, utekelezaji wa mradi huu utaenda kuondoa adha ya upatikanaji wa huduma ya umeme katika wilaya za Urambo, Kaliua na Uyui ambapo itapelekea wananchi kupata huduma bora ya umeme kwasababu mradi huo ni mahsusi kwaajili yao kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ili waweze kufurahia matunda ya juhudi ambazo serikali inafanya kuhakikisha wanapata umeme

 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.