MLANDEGE WAVUNA ALAMA 3 DHIDI YA POLISI PBZ PL

Mabingwa Watetezi Wa Ligi Kuu Soka Zanzibar Mlandege Fc Imeibuka Kidedea Baada Ya Ushindi Wa Magoli Mawili Kwa Moja Baada Dhidi Ya Polisi Zanzibar Mchezo Uliochezwa Jioni Ya Leo Katika Uwanja Wa Mao

JAPAN NA ZANZIBAR ZAAHIDI KUSHIRIKIANA

Makamu Wa Pili Wa Rais Wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla Amesema Serikali Ya Mapinduzi Ya Zanzibar Itaendeleza Uhusiano Ulipo Kati Ya Serikali Ya Japan Na Zanzibar Uliodumu Kwa Muda Mrefu.

Mhe. Hemed Ameyasema Hayo Alipofanya Mazungumzo Na Balozi Wa Japan Nchini Tanzania Yoichi Mikami Afisini Kwake Vuga Zanzibar.

Amesema Uhusiano Uliopo Kati Ya Tanzania Na Japan Utaendelea Kukuza Ushirikiano Katika Pande Zote Mbili Katika Kuimarisha Sekta Za Kilimo, Biashara, Maji Safi Na Salama, Maendeleo Ya Viwanda, Utalii Na Miundombinu Mbali Mbali.

SEKTA YA FEDHA NGUZO YA UCHUMI ENDELEVU

Waziri Wa Fedha Na Mipango Dkt. Malik Akili Amesema Sekta Ya Fedha Ni Moja Ya Eneo Litakalofanya Uchumi Wa Zanzibar Kuwa Endelevu Kama Ilivyoainishwa Katika Dira Ya Maendeleo Ya 2050.

Dkt. Malik Ameyasema Hayo Katika Ufunguzi Wa Tawi La Benki Kcb Mkunazini Zanzibar.

Katika Ufunguzi Wa Benki Hiyo, Dkt. Malik Amesema Sera Hiyo Inalenga Kuwepo Na Mageuzi Ya Kiuchumi Kwa Kuhakikisha Watu Wote Wanajumuishwa Katika Masuala Ya Kifedha Ikiwemo Huduma Za Kibenki.

Subscribe to
 

Simplenews subscription

The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.