Dkt. Mwinyi akizungumza katika shamra shamra za kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi matukufu ya mwaka 1964 katika mazoezi yaliyoanzia mnara wa muembe kisonge hadi uwanja wa amani, amesema Serikali imeamua kuimarisha viwanja vya michezo ili kufanyika michezo mbali mbali huku akiisisitiza jamii kushiriki katika vikundi vya mazoezi ili kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza.
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Tabia Maulid Mwita amesema Serikali itaendelea kuimarisha sekta ya michezo hatua kwa hatua.
Akisoma risala ya Wanamazoezi Zabesa Aviwa Juma amesema
lengo ni kuhamasisha wananchi kuepukana na maradhi.
Kamishna wa michezo Zanzibar Ameri Mohamed Ameir, ameahidi kukiendeleza chama cha mazoezi ili
kuhamasisha wananchi kupenda kufanya mazoezi.
Vikundi mia moja na hamsini 150 vimeshiriki katika mazoezi hayo na kudhaminiwa na benki ya NMB.