MTAALA WA MICHEZO KUIBUA VIPAJI TUMBATU

MICHEZO

Kurejeshwa Mtaala wa Masomo ya Michezo kwa Wanafunzi kutasaidia kuibua na kuimarisha vipaji vya Michezo mbali mbali katika jamii.

Wakizungumza katika Ziara ya Waandishi wa Habari katika Kisiwa cha Tumbatu,

Mratibu wa Michezo na utamaduni Wilaya Kaskazini 'A' Khamis Hija Mohammed na

Sheha wa Shehia ya Uvivini, Ngwali Sheha Haji, wamesema hapo awali kulikuwa na Wanafunzi waliojishughulisha na Michezo na kufanikiwa kushiriki vyema  mashindano mbali mbali.

Afisa Programu ya Michezo kutoka Chama cha Waandishi wa Habari wanawake Tamwa Zanzibar walioandaa Ziara hiyo, Khayrat Haji na Afisa Miradi Kituo cha Vijana Cyd, Rahma Ali Juma,  wamesema ziara hiyo ina lengo la kuhamasisha  umuhimu na kukuza usawa wa kijinsia kupitia Michezo kwa kuzingatia Staha, Utamaduni na Mila za eneo husika.

Msaidizi Mwalimu Mkuu Skuli ya Tumbatu Msingi 'A' Kazija Gora Khamis,  anazungumzia umuhimu wa kupatiwa mafunzo wanafunzi ili kuwajenga kushiriki Michezo tafauti. 

Wanafunzi wa Skuli ya tumbatu 'A' Msingi na Jongoe wameomba kuimarishiwa Viwanja vya Michezo sambamba na kupatiwa Vifaa vya michezo 

stories
standard
 
The subscriber's email address.
Stay informed - subscribe to our newsletter.