Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela Amewaongoza Mamia ya Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Viwanja vya Msikiti Mkuu wa Ijumaa katika Dua Maalumu ya kumuombea Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Hayati Ali Hasani Mwinyi
Akiongoza Dua hiyo Maalumu Mkuu huyo wa Mkoa amesema Hayati Mwinyi anakumbukwa kwa mengi lakini kubwa ni kwa kuwaunganisha Watanzania pamoja na kuleta Umoja wa Kitaifa.
Sheikh wa Mkoa wa Geita Al-haji Yusuph Kabaju amesema Waumini na Wananchi wa Mkoa wa Geita wameungana na Watanzania katika kumwombea heri Hayati Alli Hasani Mwinyi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita ACP Safia Jongo pamoja na Kamanda wa Jeshi la Zima moto na Uokoaji Mrakibu Hamisi Shabani Dawa, wakamkumbuka Hayati Alli Hasani Mwinyi kwa upendo wake kwa Watanzania
SHIGELA AONGOZA DUA YA KUMUOMBEA HAYATI MZEE MWINYI
standard