SHIGELA AONGOZA DUA YA KUMUOMBEA HAYATI MZEE MWINYI
Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela Amewaongoza Mamia ya Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Viwanja vya Msikiti Mkuu wa Ijumaa katika Dua Maalumu ya kumuombea Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Hayati Ali Hasani Mwinyi
Akiongoza Dua hiyo Maalumu Mkuu huyo wa Mkoa amesema Hayati Mwinyi anakumbukwa kwa mengi lakini kubwa ni kwa kuwaunganisha Watanzania pamoja na kuleta Umoja wa Kitaifa.