Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imedhamiria kuimarisha Miundo mbinu ya Barabara Mijini na Vijijini Unguja na Pemba.
Amesema malengo ya Serikali ni kuziimarisha Barabara zilizopo na kujenga mpya katika maeneo mali mbali ambapo Barabara hazijafika ili kuimarisha mtandao wa Barabara Nchini.
Akifungua Barabara ya Kijangwani-Birikau, Wilaya ya ChakeChake Mkoa wa Kusini Pemba katika shamrashamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi ya zanzibar
Dk Mwinyi amesema Serikali kupitia Wizara ya ujenzi imeingia mikataba mbalimbali na Wakandarasi kutoka Nchi tofauti kuzijenga Barabara za Mijini na Vijijini.
Aidha Serikali imetiliana mkataba na Kampuni ya CECC kwa ajili ya ujenzi wa Barabara zote za Mjini Unguja zenye urefu wa Kilomita 100.
Dk Mwinyi ameishukuru Taasisi ya Milele foundation kwa uzalendo wa kushirikiana na Serikali kukamilika kwa Barabara ya Kijangwani Birikau.