Akizungumza katika ufunguzi wa Mradi wa mfumo wa uhuwishaji na uimarishaji huduma za Maji Zanzibar huko Dimani ikiwa ni sehemu ya shamra shamra ya miaka 6o ya Mapinduzi amesema ni vyema Wananchi kuthamini juhudi hizo ili kuwa endelevu.
Aidha amewakumbusha Wananchi hao kuendelea kupanda Miti ili kuhifadhi Mazingira ya maeneo hayo ya Maji pamoja na kuhakikisha wanadhibiti umwagikaji ovyo wa Maji ili kuepuka kukosesha wengine huduma hiyo
Waziri wa Maji ,Nishati na Madini Mh Shaibu Hassan Kaduara amewaomba Wananchi kuchangia huduma za Maji kupitia Miradi mbali mbali inayoendelea kujengwa ili kuimarisha huduma hizo
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Maji Zanzibar Dk Salha Kassim amesema mradi huo wa kisasa ni Mkombozi wa Wananchi kwani utawaondoshea usumbufu katika upatikanaji wa huduma hiyo
Mradi huo uliohusisha ujenzi wa Visima na Matangi ya kuhifadhia Maji kwa maeneo matatu tofauti umeharimu zaidi ya dola milioni 90 ambapo utanufaisha jumla shehia 36.