RAIS MSTAAFU WA ZANZIBAR MH AMANI KARUME AMESEMA UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI NI SEHEMU YA KUTIMIZA DHAMIRA YA MAPINDUZI
Akizungumza katika ufunguzi wa Mradi wa mfumo wa uhuwishaji na uimarishaji huduma za Maji Zanzibar huko Dimani ikiwa ni sehemu ya shamra shamra ya miaka 6o ya Mapinduzi amesema ni vyema Wananchi kuthamini juhudi hizo ili kuwa endelevu.
Aidha amewakumbusha Wananchi hao kuendelea kupanda Miti ili kuhifadhi Mazingira ya maeneo hayo ya Maji pamoja na kuhakikisha wanadhibiti umwagikaji ovyo wa Maji ili kuepuka kukosesha wengine huduma hiyo