WAFANYABIASHARA SOKO LA KINYASINI WALIA NA MIUNDOMBINU ISIYO RAFIKI
Wafanyabiashara wa Soko la Kinyasini Wilaya ya Kaskazini 'a' Unguja wamesema kuwa Eneo la Soko ni dogo kwa kufanyia biashara zao na linasababisha msongamano baina ya Wafanyabiashra na Wateja.
Wakizungumza na Kamera ya Biashara na Uchumi ZBC Wafanyabiashara hao wamesema Soko hilo halikidhi kuchukua Watu wengi hali inayopelekea baadhi ya Wafanyabiashara kupanga bidhaa chini na pembezoni mwa barabara.

